Kim Kardashian ndiyo nani? Inaonekana kama 2014 umekuwa mwaka wa Lupita Nyong’o!
Ni miezi kadhaa tu imepita tangu achukue tuzo ya Oscar kama mwigizaji wa kike msaidizi kwa kufanya vizuri kwenye filamu ya 12 Years a Slave, nyota huyo wa Hollywood ametokezea kwenye ukarasa wa mbele wa jarida la Vogue.
Akiwa amevalia gauni, nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, mzaliwa wa Kenya anaonekana kutokuchoka baada ya kutolewa Julai kwenye mitindo ya Biblia.
Akiwa kwenye mahojiano,Nyong’o alizungumzia kuhusu umaarufu na kudai kuwa hajihisi kuchanganyikiwa anapokuwa kwenye umma unaomzunguka.
“Inaonekana kama tasnia ya burudani imevamia katika maisha yangu”, alisema Lupita.
“Watu walioonekana kuwa mbali na mimi ghafla nawaona mbele yangu na kudai kunijua – kabla ya mimi kuwajua”.
“Hata kwenye ndoto zangu za kuwa muigizaji, ndoto yangu haikuwa umaarufu. Ndoto yangu ilikuwa ni kufanya nilichotaka kufanya”.
Wasanii wa kike Tanzania
Dada zetu akina Wema Sepetu, Kidoti, Aunty Ezekiel, Irene Uwoya, mnajitahidi sana lakini haitoshi, Lupita ni mtu wa kumfanya kioo na kumuangalia anachofanya, sio lazima uige kila kitu, msifanye mambo ya kutafutwa na magazeti ya udaku, mjitahidi hata tuwaone kwenye majarida makini ya Kenya tu, itakuwa heshima kwenu, japo kidogo.
Kumbuka hayo hayaletwi na skandali za kipuuzi, bali kazi, nidhamu, ubunifu, kujituma na nyavu kazi, jengeni mahusiano ya kudumu na wasanii wa kimataifa, sio ya kimapenzi bali ya ari ya kutaka kuvuka milima ya mafanikio, mjifunze wazungu husema ‘Think globally, act locally’
Kingine elimu, Lupita Nyong’o kasomea shahada ya uzamivu (master’s degree) ya uigizaji kwenye moja ya Chuo cha heshima Marekani na duniani cha Yale, hajacheza filamu nyingi kuwazidi nyinyi, hazifiki hata tano, tulizeni akili zenu mtathmini nyayo zake, mtajifunza mengi muhimu kutoka kwake kwa manufaa yenu. Ukiacha kujifunza, umeacha kuishi.

0 comments:
Post a Comment