Facebook

Saturday 13 September 2014

Asilimia 52 ya wanawake Tanzania hutumia vipodozi vyenye sumu


Zaidi ya asilimia 52 ya wanawake
hutumia vipodozi vyenye sumu
ambavyo huwasababishia matatizo
mbalimbali ikiwamo kansa ya ngozi,
figo pamoja na kuharibika kwa mimba
kwa mama mjamzito. Aidha katika
utafiti uliofanywa na Asasi
isiyokuwa ya kiserikali Envirocare
mwaka jana inaonyesha mikoa ambayo
imeathirika zaidi na matumizi ya
vipondozi hivyo ambayo ni Tanga,
Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma,
Arusha, Mbeya na Kilimanjaro.
Meneja wa Mradi huo, Elfansia
Shayo, alisema Envirocare imeandaa
kampeni kwaajili ya kupinga
matumizi ya vibodozi hivyo
itakayofanyika leo jijini Dar es
Salaam. “Envirocare kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Chakula
na Dawa Tanzania (TFDA) imefanya
utafiti ulionyesha zaidi ya
asilimia 52 ya watumiaji wa
vipodozi hivyo ni wanawake na
baadhi yao wanajua madhara yake,”
alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo,
Loyce Lema, alisema kampeni hiyo
inahusu kutoa elimu kwa jamii
kuhusu matumizi ya vipodozi hivyo
na ambazo viambato hivi husababisha
madhara kwa watumiaji na mazingira.
Alisema pamoja na TFDA kuweka mfumo
thabiti wa udhibiti wa vipodozi
ambao unatumia njia mbalimbali
ikiwamo usajili wa vipodozi, utoaji
wa vibali vya biashara, na ukaguzi
wa maduka bado mfumo huo
unachangamoto kwani vipodozi
vimekuwa vikiingizwa nchini kwa
kutumia njia zisizo rasmi.

CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment