Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Tuesday, 19 August 2014

Baada ya kubwaga manyanga ITV na Redio One,Maulid Kitenge atimkia EFM RADIO


Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge amesaini Mkataba wa kazi na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7
kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam.

 
Katika picha hapo juu,Kushoto ni Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela. Mtangazaji mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM
93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam leo. 

 
 Hapo juu ni barua aliyoiandika Maulidi Baraka Kitenge kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa ITV/RADIO ONE akijiuzulu nafasi aliyokuwa nayo katika kampuni hiyo.
 
 Hapo juu,hiyo ni tweet ya Maulid Baraka wa Kitenge aliyoipost baada ya kuacha kazi IPP

Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndiye mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.
“Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasaini mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo

Endelea kutembelea www.bantutz.com.Usisahau kumjulisha mwenzio BantuTz.com imerudi tena.

ATLETICO MADRID vs REAL MADRID.SUPERCOPA DE ESPSNA.Simeone apiga mkwara mzito.


Meneja mwenye mbwembwe na hisia kubwa katika soka wa Mabingwa wa La Liga msimu uliopita Atletico Madrid,DIEGO SIMEONE amesisitiza tofauti kubwa kati ya timu yake Atletico Madrid na Real Madrid ni za kiuchumi tu na pia kudai timu yake ipo imara licha ya kumpoteza Straika wao mkubwa Diego Costa aliehamia Chelsea.

Akiongea na Waandishi wahabari kabla Atletico kuivaa Real kwenye Mechi ya Kwanza ya Supercopa de Espana itakayochezwa Jumanne Usiku huko Santiago Bernabeu ikiwa ni mechi inayowakutanisha tena baada ya ile fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa Mei huko Lisbon, Ureno na Real kuifungaa Atletico magoli 4-1.

Diego Simeone, ambae ndie Kocha Mkuu wa Atletico, amesema: “Sie tumenunua Wachezaji 7 au 8 kwa Euro Milioni 95 wao wametumia Euro Milioni 95 kununua Wachezaji Watatu tu!” 

 Baadhi ya Wachezaji waliowanunua Atletico, ambao ndio Mabingwa wa Spain, ni pamoja na Antoine Griezmann na Mario Mandzukic, na Real,Mabingwa wa Ulaya, wamenunua Wachezaji Watatu tu ambao ni James Rodriguez, Toni Kroos na Keylor Navas. 

Simeone amesisitiza: “Klabu yetu ina ubunifu. Sisi tunacheza Kitimu na si Wachezaji 11 tu, ni Kundi la Wachezaji 18 au 20.”  

Supercopa de Espana ni Kombe linalogombewa na Bingwa wa La Liga na Mshindi wa Copa del Rey na Msimu uliopita Atletico Madrid ndio walikuwa Mabingwa wa La Liga na Real Madrid kutwaa Copa del Rey.

Msimu uliopita Timu hizi zilikutana mara 5, ikiwemo hiyo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, na pia Real kuichapa Atletico Jumla ya Bao 5-0 katika Mechi mbili za Nusu Fainali ya Copa del
Rey na kutinga Fainali ambayo waliifunga Barcelona na kutwaa Kombe.


Lakini kwenye La Liga, Atletico walimudu kuifunga Real Mechi moja na kutoka Sare Mechi nyingine na hatimae kutwaa Ubingwa.
Wiki iliyopita, Real wameanza tena kwa moto baada ya kuichapa Sevilla, Mabingwa wa UEFA EUROPA CUP, magoli 2-0 huko Cardiff, Wales na kutwaa UEFA Super Cup huku magoli yote yikifungwa na Cristiano Ronaldo.Mechi hizi za Supercopa de Espana huashiria kuanza kwa simu mpya wa Soka huko Spain
ambako La Liga itaanza rasmi Wikiendi ya Agosti 23.


NI MECHI MBILI AMBAZO ZITACHEZWA KUMPATA MSHINDI
MECHI YA KWANZA ITAPIGWA.J'NNE 19 AGOSTI SAA 5:59/23:59 (MASAA YA AFRIKA MASHARIKI)
Real Madrid v Atletico de Madrid [El Estadio Santiago Bernabeu]

MECHI YAPILI ITAPIGWA.IJUMAA 22 AGOSTI.SAA 5:30/23:30(MASAA YA AFRIKA MASHARIKI)
Atletico de Madrid v Real Madrid [Estadio Vicente Calderon]


Endelea kutembelea www.bantutz.com.Mwambie mwenzio BantuTz.com imerudi.Sambaza upendo.

Chelsea yaanza Ligi kwa ushindii mnono.


Chelsea imeanza Ligi Kuu England kwa ushindi wa Ugenini huko Turf Moor dhidi ya Timu iliyopanda Daraja Burnley ambayo
wameifunga magoli 3-1 magoli yote ya Mechi hii yalifungwa Kipindi Cha Kwanza lakini ni Burnley ndio walitangulia kufunga kwa goli lililofungwa na  Shucott Arfield dakika ya 14 na Diego Costa akicheza Mechi yake ya kwanza ya Ligi, kusawazisha Dakika ya 17.


Goli la Pili la Chelsea lilifungwa na Andre Schurrle Dakika ya 21 na Branislav Ivaovic kupiga Bao la 3 Dakika ya 34.Ni mwanzo mzuri kwa The blues katika kampeni yao ya kutafuta taji msimu huu baada ya kutoka kapa msimu uliopita

Endelea kutembelea www.bantutz.com.Mwambie mwenzio BantuTz.com imerudi.

Barcelona yaua 6,Suarez acheza kwa mara ya kwanza na kupokewa kwa Shangwe.

Kwenye Mechi ya kila Mwaka inayochezwa Uwanja wa Nou Camp kabla Msimu mpya kuanza kugombea Kombe la Joan Gamper ili kumtukuza Joan Gamper aliekuwa Mwanzilishi, Mchezaji na
baadae Rais wa Barcelona, FC Barcelona iliifunga Klabu ya Mexico Club Leon magoli 6-0 na kutwaa Kombe lao hilo.
 

Hii ilikuwa Mechi ya kwanza kwa nyota wa Brazil Neymar kucheza tangu aumizwe Mgongoni kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwanzoni mwa Julai huko Nchini Brazil wakati
akiichezea Brazil ilipokutana na Colombia. 


Luis Suarez, ambae amehamia Barcelona kutoka Liverpool lakini yupo kwenye Kifungo cha FIFA cha Miezi Minne, aliingizwa zikibaki Dakika 13 kumbadili Rafinha na kupokewa kwa shangwe
kubwa katika Mechi yake ya kwanza kwa Barca.Suarez alilegezewa Kifungo hicho na CAS,Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, na kuruhusiwa kufanya Mazoezi na kucheza Mechi
za Kirafiki.Lionel Messi aliipa Barcelona Bao la Kwanza
kwenye Dakika ya 3 tu kufuatia ushirikiano mwema kati ya Rakitic, Messi na Neymar ambae alimrudishia Messi aliefunga.
Bao la Pili lilifungwa na Neymar katika Dakika ya 12 kutokana na pasi safi ya Iniesta na akaongeza Bao la 3 Dakika ya 44 baada pasi murua ya Messi.


Hadi Mapumziko Barcelona 3-0 Club Leon .Kipindi cha Pili, Barca waliongeza Bao nyingine 3 zilizofungwa na Munir El Haddadi, Dakika ya 55 na 78, na moja la Sandro Ramírez, Dakika ya 89.


Endelea kutembelea www.bantutz.com.Mwambie mwenzako BantuTz.com imerudi tena.

Monday, 18 August 2014

ALICHOKISEMA ANCELOTI KUHUSU UHAMISHO WA DI MARIA

Kutokana na tetesi mbalimbali zinazomhusu winga hatari Angel Di Maria kuhamia katika klabu ya Manchester United inayomuhitaji kwa udi na uvumba.
Meneja wa Real Madrid aliamua kuvunja ukimya na kusema haya "Sitaki kuliingilia
suala la Di Maria, kwa sababu litanipotezea
umakini wangu kuelekea mchezo dhidi ya Atletico.
Sijui mpaka sasa ameamua nini kuhusu hatma
yake, ninachofahamu yupo tayari kucheza, na
mpaka kufikia August 31 anaweza kuendela
kuwa hapa. Ikiwa mpaka wakati huo wa
dirisha la usajili litakapofungwa - akiendelea
kuwa hapa au asipokuwepo, tutalifikiria suala
hilo baadae."

Endelea kutembelea www.bantutz.com....Mtaarifu mwenzako mwambie tumerudi tena katika muonekano bora zaidi.

Wednesday, 6 August 2014

Yanga wafunguka baada ya kuondolewa kwenye Michuano ya Kombe la Kagame

Uongozi wa klabu ya Young Africans leo
umefanya mkutano na waandishi wa habari
juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa
michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza
sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno
Njovu amesema walipata barua ya mwaliko
wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014
na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa
kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao
kuiwasilisha kwa CECAFA.
"Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano
hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya
wachezaji na viongozi ambao watasafiri
kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano
hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na
sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza"
alisema Beno.
Lakini katika hali ya kushangaza jana
tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA
imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa
kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya
Azam kuchukua nafasi yetu "aliongeza Beno."
Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji
wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni
lazima wawe na leseni za kucheza mpira
kutoka kwa chama husika, jambo ambalo
ambalo orodha tuliyowapelekea wachezaji
wote wataichezea Yanga msimu huu wa
2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya
kikosi ambacho kingekwenda kushiriki
michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza
ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua
dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua
kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua
na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka
timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji
watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya
kocha Leonado Neiva ambaye amekua na
wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa
klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine
kwa kusema kikosi kilichopelekwa
hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu
Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya
kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo
Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho
kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu
uliopita Hans ilitoa maelekezo ya kupunguza
wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili
kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya
kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika
idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita.
b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na
majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa
Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19,
2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani
miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata
muda wa kupumzika.
c) Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia
kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake
watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda
na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda
wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye
timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha
kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.
d) Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya
kufanyia kazi nchini, uhamisho wa Kimataifa
(ITC) ili waweza kushiriki michuano ya
Kagame, na moja ya kanuni za CECAFA
mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni
lazima awe na leseni ya kucheza mpira kwa
ligi ya ndani.
e) Katika wachezaji 20 waliochaguliwa
kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6
wamepandishwa moja moja katika kikosi cha
wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi ya
wachezaji wa U20 kuwa watano tu.
f) Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars
kwa takribani miezi mitatu bila ya kupumzika,
daktari alipendekeza wapate japo siku kumi
na nne (14) za kupumzika ili miili yao iweze
kupoa na kuanza upya tena maandalizi ya
msimu mpya.
g) Yangga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi
ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi
cha kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na
wachezaji mda wote na kujua ubora wa
wachezaji wake.

Monday, 4 August 2014

TETESI ZA USAJILI KATIKA MAGAZETI MBALIMBALI BARANI ULAYA NA BantuTz.com


Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers
amesema hana mpango wa kumchukua Mario
Balotelli kutoka AC Milan, baada ya mchezaji
huyo kuhusishwa na Anfield (Daily Mirror),

>Manchester City wanakaribia kukamilisha
usajili wa beki wa Porto Eliaquim Mangala,
23, kwa pauni milioni 32 (Manchester
Evening News),

>Tottenham wapo karibu
kufikia makubaliano na Villareal kumsajili
beki wa kati Mateo Musacchio, 23, (Times),

>Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino
anataka kuwapa Southampton winga Nacer
Chadli ili kuwashawishi kumchukua Morgan
Schneiderlin (Sun),

>Meneja wa West Ham Sam
Allardyce anataka kumchukua winga wa
Manchester United, Wilfried Zaha, 21 (Sun),

>West ham pia wanamtaka Peter Crouch, 33,
kutoka Stoke City kuziba pengo la Andy
Carroll ambaye ni majeruhi (Daily Express),

>Meneja wa Southampton, Ronald Koeman
anataka kumsajili winga chipukizi wa
Manchester United Demetri Mitchell kwa
mkopo (Daily Mirror),

>AC Milan wanamtaka
kipa wa Liverpool Pepe Reina, lakini kipa
huyo anataka mshahara mkubwa (Daily Mail),

>Meneja wa Crystal Palace, Tony Pulis
anamyatia beki wa Stoke Marc Wilson (Daiky
Star),

>Newcastle wana matumaini ya kumsajili
beki wa kati kutoka Nottingham Forest
Jamaal Lascelles, 20, kwa pauni milioni 3
(Daily Mirror),

>Tottenham wanafikiria
kumchukua Samuel Eto'o, 33, baada ya
kuondoka Chelsea (Tuttosport),

>Liverpool
wanakaribia kumsajili Alberto Moreno, 22
kutoka Sevilla kwa pauni milioni 16 (AS),

>kiungo Marco Reus, 25 ambaye amehusishwa
na kwenda Bayern Munich na Liverpool
atabakia Borussia Dortmund kwa msimu
mwingine (L'Equipe),

>Mkataba wa pauni
milioni 60 kati ya Real Madrid na Paris St-
Germain juu ya winga kutoka Argentina Angel
Di Maria huenda ukakamilika katika siku
mbili zijazo (Marca),

>Liverpool imetoa dau la
pauni milioni 5 kutaka kumsajili beki wa
Barcelona Dani Alves, 31 (Mundodeportivo),

>Wolfsburg wanamtazama mshambuliaji wa
Chelsea Fernando Torres, 30, baada ya
kushindwa kumchukua Romelu Lukaku, 21
aliyekwenda Everton (Bild),

>Real Madrid
wanataka kumchukua kiungo wa Wolfsburg
Luiz Gustavo, 27 iwapo Sami Khedira
ataondoka. Arsenal na Chelsea wanamfuatilia
kiungo huyo (Bild),

>Beki wa kati kutoka
Brazil, Miranda amekataa kwenda Cheslea,
Manchester United na Barcelona, na badala
yake atasalia Atlètico Madrid (Marca),

>Juventus wanaonekana kukata tamaa ya
kumzuia Arturo Vidal baada ya Manchester
United kutoa pauni milioni 40. Mabingwa hao
wa Italia watamtaka Nani na Javier Hernandez
katika mkataba huo (Corriere dello Sport).

By Katemi Methsela

Source:www.bantutz.com

ORODHA YA VIWANJA VYA NDEGE VYA KIMATAIFA 5 BORA ZAIDI AFRIKA....

1. OR TAMBO INTERNATIONAL AIRPORT  (ORTIA), JOHANNESBURG - AFRIKA KUSINI.

Kiwanja hiki ndicho kiwanja bora zaidi Afrika na kina uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu Milioni 17 kwa mwaka na kwa sasa kiwanja hiki kimefanyiwa marekebisho na kuongezwa miundo mbinu na kukifanya kiweze kuhudumia zaidi ya abiria Milioni 28 kwa mwaka.
Hata hivyo, ORTIA ndicho kiwanja kikubwa zaidi cha ndege kilicho na pilikapilika nyingi kabisa Afrika na pia kiwanja hiko kina wafanyakazi zaidi ya 18,000 walioajiriwa kiwanjani hapo na makampunim tofauti tofauti. Jina la kiwanja hiko limetokana na aliyekuwa akipinga masuala ya ubaguzi wa rangi Afrika ya kusini kipindi cha makaburu aliyejulikana kama Oliver Reginald Tambo kama kumuenzi.

2. CAPE TOWN INTERNATIONAL AIRPORT, CAPETOWN - AFRIKA KUSINI.


Kiwanja hiki kipo Capetown Africa ya kusini na ifikapo mwaka 2015 kitakuwa kina hudumia zaidi ya Abiria Milioni 14 na pia kiwanja hiki hutumika sana kwa ajili ya shughuli za kitalii kwasababu mji wa Capetown una vivutio vingi vya utalii nchini humo.

3. KING SHAKA INTERNATIONAL AIRPORT, DURBAN - AFRIKA KUSINI

Kiwanja hiki kilifunguliwa mnamo mwezi Mei 2010 na pia kina julikana kwa jina la LA MERCY AIRPORT, kipo kilometa takriban 35 kaskazini kutoka katika mji wa Durban. Pia inasemekana kiwanja hiki kina ukubwa mara tatu zaidi ya Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Durban (Durban International Airport).

4. CAIRO INTERNATIONAL AIRPORT, CAIRO - MISRI


Hiki ni kiwanja cha ndege kikubwa zaidi Misri, ni cha pili kwa kuwa na pilika pilika nyingi za watu na zaidi ya ndege 65 hutumia kiwanja hiko kwa mwaka.


5. HURGHADA INTERNATIONAL AIRPORT, HURGHADA - MISRI

Kiwanja hiki kinajengo la abiria moja tu ambalo linafanya kazi kwa sasa, pia linaongezwa jengo lingine la abiria ambalo litakifanya kiwanja hiki kiweze kuhudumia zaidi ya abiria milioni 7.5 kwa mwaka.
Hata hivyo ni zaidi ya ndege 40 hutumia kiwanja hiki kwa mwaka.
- ngastuka