Facebook

Sunday, 20 April 2014

Kali ya Mwaka.....waumini Nchini Kenya wasafisha lami kwa kuideki.................fuatilia hapa kioja hiki............................

Screen Shot 2014-04-20 at 1.08.01 AM 
 Wakazi wa  jiji la Eldoret nchini Kenya wamemfanya kila anayeliona hili kustaajabishwa na kutaka kujua chanzo cha wao kufanya hivi baada ya kujitolea  kupiga deki barabara ya lami ya Oginga Odinga jijini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya. 
Wanasema  wameamua kufanya hivi ikiwa ni maandalizi ya kumlaki nabii Daktari Awuor kwa ajili ya maombi ya leo na siku ya Jumatatu kuadhimisha pasaka na kumshukuru jehova kwa kuwasaidia jiji la Eldoret kufanyika uchaguzi wa amani mwaka 2013 
Hata hivyo maoni mbalimbali yaliyotolewa na Wakenya kuhusiana na tukio hil; maoni mengi yameonekana kupinga kitendo cha waumini hao wa kanisa la Jesus is lord kwa kumpa Daktari Awuor heshima kupita kiasi.
Mkurugenzi mkuu wa Kass media inayo miliki Radio ya kass fm inayotangaza kwa lugha ya kikalenjin inayozungumzwa na wakazi wa jiji la Eldoret Julius lamaon, amesema ‘watu wetu waache kupotoka, jiji letu limebadilishwa na kuwa jiji la vituko…… Gavana hatakiwi kuhudhuria mkutano huu

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kufahamu matukio mbalimbali ya kustaajabisha yanayotokea duniani....................

0 comments:

Post a Comment