Sunday, 27 April 2014
Jaji Warioba atoa ya Moyoni dhidi ya Uongo na Matusi Bunge la Katiba........
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wametumia vibaya Bunge hilo kwa kumshambulia na kumsingizia mambo ya uongo kwa makusudi, akisema matusi yanayotolewa dhidi yake yanamuumiza.
Aidha, Warioba amesema ingawa haelewi kwa nini wanaomshambulia wameamua kutumia lugha za matusi dhidi yake binafsi, hatajutia kuchaguliwa kuiongoza tume hiyo kwa kuwa ilikusudia kuwaletea maendeleo wananchi wote kwa kuwapatia Katiba wanayoitaka.
Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja wakati baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na viongozi wa CCM wakiikosoa Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba kwa maneno makali,huku wakimshutumu na kumkejeli yeye na baadhi ya wajumbe wa tume aliyoiongoza.
Related Posts:
Rais Dkt Magufuli apokea hati ya makabidhiano ya Ofisi ya Ikulu kutoka kwa Rais Mstaafu Dkt Kikwete leoPicha:-Rais Dk MagufuliJP akipokea hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu Dk J M. Kikwete Ikulu Dar leo. … Read More
Viti Maalum: BAWACHA Ruvuma wampa Mh. Mbowe siku 3.BAWACHA Mkoani Ruvuma wampa Mwenyekiti Mbowe siku tatu kutengua uamuzi wa kumteua Zubeda Sakuru Ubunge Viti Maalum, wasikitishwa na uteuzi huo wadai ni wa upendeleo-Aidha wameshangazwa na uongozi wa Chama kutotokea kwenye kik… Read More
Dkt Slaa atoa tathmini ya maamuzi anayofanya Rais Dkt Magufili.Aliyekuwa katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa ametoa tathmini yake kwa siku chache za Rais John Magufuli alizoanza kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano na maamuzi aliyoyafanya. Dkt. Slaa ambaye alikuwa mgombea u… Read More
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya apiga marufuku matumizi ya simu za mkononi wakati wa kaziMkuu wa mkoa wa Mbeya amepiga marufuku matumizi ya simu za mkononi wakati wa kazi mkoani Mbeya ili watumishi wa serikali na mashirika ya umma wahudumie jamii kwa wakati. Asisitizia marufuku mtandao wa WhatsApp, ataka wa… Read More
Bantuz MAGAZETINI-Soma kilichoandikwa katika Magazeti ya leo Novemba 12. BantuTz MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusoma na kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata ha… Read More
0 comments:
Post a Comment