Tuesday, 29 April 2014
Mwanachuo afia chumbani kwa hawara yake...........
MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa miaka 20, mwanafunzi wa Chuo cha Eden Hill kilichopo Kwamfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani kwa mtu anayetajwa kuwa ni hawara yake, Hafidh Mohammed.
Tukio hilo lilitokea April 26, mwaka huu na kukusanya umati huku mwanaume aliyelala na binti huyo akitokomea kusikojulikana.Marehemu anadaiwa kuwa mwenyeji wa Makambako mkoani Njombe.
Akizungumza na waandishi wetu juzi Kibaha, mama wa Hafidh ambaye pia ni mjumbe wa eneo hilo, Zainabu Saidi alisema mwanaye alimweleza kutokea kwa tukio hilo asubuhi kulipokucha na kabla ya hapo, hakuwa akifahamu kama alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo kwa vile aliyekuwa akimfahamu ni mwanamke mwingine ambaye alizaa naye.
“Mimi kwa kweli sikuwa na taarifa yoyote juu ya uhusiano wao na huyu mwanafunzi, nimeletewa taarifa asubuhi na kijana wangu huku akionekana kuchanganyikiwa, nimejaribu kumsihi asikimbie lakini imeshindikana,” alisema mama huyo.
ALIVYOAGA CHUONI
Wanafunzi wa chuo hicho kinachofundisha masomo ya biashara na habari ambao walikataa kutaja majina yao waliliambia gazeti hili kuwa, marehemu Atu aliwaaga anakwenda jijini Dar es Salaam kumuuguza wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Amana, Aprili 23, mwaka huu.
Hata hivyo, walisema uondokaji wake uliwapa maswali mengi kwani tofauti na walivyotegemea kuwa angebeba mfuko mkubwa wenye nguo za kubadili, yeye aliondoka akiwa na mkoba wake wa mkononi pekee hali iliyoonesha hakuwa akienda mbali.
Walisema siku tatu baadaye walipatwa na mshtuko mkubwa baada ya mlinzi wa hosteli yao kuwaletea taarifa za kifo cha mwenzao kilichotokea katika chumba cha mvulana huyo anayeishi jirani.
MAJIRANI NAO WANENA
Majirani waliozungumza na gazeti hili walisema kwao haikuwa mara ya kwanza kumuona msichana huyo, kwani mara kwa mara alikuwa akifika pale ingawa akishaingia ndani hakuwa akitoka nje.
Walisema mara zote hizo, mwanaume huyo mwenyeji ndiye alikuwa akitoka nje na kwenda kumnunulia chakula.
POLISI WAUPELEKA MWILI HOSPITALI YA TUMBI
Jeshi la polisi liliwasili eneo la tukio na kuukuta mwili huo ukiwa umelala kitandani ukiwa hauna jeraha, lakini pembeni yake kulikutwa vidonge ambavyo havikufahamika ni vya aina gani ambavyo pia vilichukuliwa pamoja na mkoba wake hadi kituonis.
Minong’ono kutoka kwa majirani kuhusiana na vidonge hivyo ilitofautiana, baadhi yao walisema huenda vilitumika katika jaribio la kutoa mimba, wengine walisema inawezekana msichana huyo alipata ugonjwa wa ghafla usiku na mwanaume huyo alikwenda kumchukulia vidonge hivyo ambavyo havikuweza kumsaidia marehemu kupata nafuu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Ulrrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema juhudi za kumtafuta mwanaume huyo zinaendelea huku madaktari nao wakiendelea na uchunguzi wao ili kubaini chanzo cha kifo hicho
Related Posts:
Unyama !! Kijana amkata kichwa Mdogo wake ili apate utajiri huko Morogoro UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni! Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamng’ang’ania mfanyabiashara maarufu wa Wilaya ya Mvomero, Johnson Damian Mkude (39) akituhumiwa kumkata kichwa mdogo wake wa kuzaliwa, Mathi… Read More
Unyama!! awachoma watoto wake mikono ! Watoto wanaodaiwa kufanyiwa ukatili wakionyesha vidonda kwenye mikono yao ambavyo vinatokana na kuchomwa moto na baba ya mzazi nyumbani kwao Mbagala Kibondemaji jijini Dar es Salaam jana. Vitendo vya ukatili dhidi yawatoto … Read More
Kisima cha maajabu Dodoma.Maji yake Koo mbili za Wanyazaga na Wambukwa Mnyambwa wakiwa wamekusanyika kukizunguka kisima kinachosemekana kimejaa maajabu cha Bwibwi kilichopo Katika kijiji cha Iyumbu kilichopo pembezoni mwa Chuo kikuu cha Dodoma [UDOM] B… Read More
Imebainika ni Kweli majina ya waliofaulu ule usaili wa Uhamiaji yalichakachuliwa. Wiki kadhaa zimepita kumekuwa na Habari kuhusu Majina ya Waliofauli Usaili wa Nafasi ya Ukonstebo Pale Uhamiaji ambayo ilisemekana yalikuwa yamechakachuliwa kwani wengi waliopata kazi hiyo walikuwa na undugu na wafanya… Read More
Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu{HESLB} yahaidi kulipa fedha kwa Wanafunzi wa Vyuo vikuu,Walioomba mikopo nao kushughulikiwa. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB),imesema mwishoni mwa wiki hii, itakuwa imelipa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ambao hawajapata fedha hizo kwa mwaka 2013/14. Mkurugenzi Msaidizi wa Haba… Read More
0 comments:
Post a Comment