Facebook

Wednesday, 30 April 2014

Unakijua alichokisema Guardiola baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Mdrid jana.........fuatilia hapa.

397592_heroa
PEP Guardiola ameeleza kuwa kiwango walichoonesha Bayern Munich ni kikubwa mno japokuwa walifungwa mabao 4-0 na Real Madrid katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya UEFA kwenye uwanja wa Allianz Arena jana.
The Bavarians walichanganyikiwa kwa mabao mawili ya Sergo Ramosi na Cristiano Ronaldo na kuvuliwa ubingwa kwa wastani wa mabao 5-0 kufuatia kupigwa bao 1-0 mchezo wa kwanza Santiago Bernabeu.

Guardiola ambaye kikosi chake kilicheza kwa kujituma zaidi katika kipigo cha kwanza cha bao 1-0 Bernabeu, hakikuweza kufua dafu jana Allianz Arena.

“Kila kitu kinatokea katika mpira kutokana na kucheza vizuri. Nimefungwa mara nyingi katika kazi yangu na hii ni mojawapo”. Guardiola amewaambia waandishi wa habari.

“Tulifungwa mabao mengi, lakini tulicheza kwa kiwango kikubwa na ndio sababu ya kupoteza”.

“Hakuna sababu nyingine, huu ndio mpira”.

“Unapocheza vibaya, unafungwa mabao mengi. Tuliingia na nguvu, tungeweza kufunga kwa nafasi tulizopata, lakini hatukuweza”.

“ Kucheza kwetu vibaya ndio sababu pekee ya kufungwa”.

Bayern imefanikiwa kutwaa kombe la dunia la klabu na Bundesliga msimu huu, na wamebakiwa na kombe la mwisho la DFB-Pokal mei 17 dhidi ya Borussia Dortmund.

Hii itakuwa kama marudio ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka jana

Related Posts:

  • Nguli wa Real Madrid afariki dunia.   Mchezaji nguli wa Real Madrid Alfredo Di Stefano, anayetajwa kuwa mmoja wa wachezaji wazuri duniani amefariki dunia. Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid aliyekuwa na umri wa miaka 88 alipatwa na mshtuko wa moy… Read More
  • Scolari "Tutashinda bila Neymar" Kocha wa Brazil Luiz Filipe Scolari amesema vijana wake wataweza kucheza bila ya mshambuliaji wake aliyeumia, Neymar, watakapocheza na Ujerumani siku ya Jumanne katika nusu fainali ya Kombe la Dunia. Neymar amepa… Read More
  • Louis Van Gaal aongeza kocha mwingine kwenye benchi lake la ufundi.   Louis Van Gaal amemuongeza kocha wa team ya taifa ya vijana ya Uholanzi U-21 katika benchi la ufundi la Manchester United. Albert Stuivenberg atakua kocha wa tatu wa kiuholanzi kujiunga kuifundisha Manchester… Read More
  • 5 BORA YA JEZI ZENYE MDHAMINI GHALI DUNIANI. 1. Manchester United(CHEVLORET)-$80 Million 2. Barcelona(Qatar Airways)-$45 Million 3. Bayern Munich(Deutsche Telekom)-$40 Million 4. Real Madrid((Fly Emirates)-$39 Million 5. Liverpool(Standard Chartered)-$31 Million … Read More
  • Uholanzi kumenyana na Argentina Wachezaji wa Uholanzi Arjen Robben na Dirk Kuyt Uholanzi imeishinda Costa Rica katika mikwaju ya penalti ili kuungana na Argentina,waandalizi wa michuan… Read More

0 comments:

Post a Comment