Facebook

Wednesday, 30 April 2014

Adnan Januzaj ahakikishiwa nafasi Ubelgiji katika fainali za kombe la dunia Brazil...

ADNAN_JANUZAJ-IN_RED


















CHIPUKIZI wa Manchester United, Adnan Januzaj, atakuwemo kwenye Kikosi cha awali cha Kombe la Dunia cha Belgium kama ilivyohakikishwa na Kocha wa Nchi hiyo Marc Wilmots.
Wiki iliyopita, Marc Wilmots ndie alietoboa kuwa Januzaj amekubali kuichezea Belgium licha ya kutakiwa na kuwa na uwezo wa kuziwakilisha Albania, Kosovo, Turkey na Serbia kwa misingi ya mizizi ya Asili ya Wazazi wake.
Januzaj atakuwemo kwenye Timu ya Belgium ambayo itapiga Kambi ya Mazoezi Mwezi ujao kujitayarisha na Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa huko Brazil kuanzia Juni 12 lakini Kocha Marc Wilmots amesema hivi sasa hawezi kuahidi kama Kinda huyo atakuwemo kwenye Kikosi cha mwisho cha Wachezaji 23 watakaoenda Brazil.
Kocha huyo amesema: “Nimemuona mara kadhaa akicheza na sasa nataka kumuona akiwemo kwenye Kikosi changu. Atakuwemo kwenye Kikosi cha Awali cha Wachezaji 30 na atakuwepo kwenye Kikosi cha Wachezaji 26 au 27 ambao watafanya Mazoezi huko Genk na baadae Sweden. Napenda kuwa na idadi ndogo ya Wachezaji lakini Januzaj atakuwemo.”
Januzaj, mwenye Miaka 19, alijiunga na Manchester United Mwaka 2011 akitokea Anderlecht na Msimu huu amepandishwa na kuwemo Kikosi cha Kwanza cha Timu hiyo na Mechi yake ya kwanza ilikuwa ya Ngao ya Jamii ambayo Man United waliibwaga Wigan 2-0 Mwezi Agosti Uwanjani Wembley.
Tangu wakati huo amecheza Mechi 32 na kuifungia Man United Bao 4.
Kocha Wilmots alifafanua kuwa alipokutana na Januzaj  na Mawakala wake aliwaambia wazi kuwa uamuzi wa Mchezaji huyo kuwemo kwenye Kikosi kitakacho kwenda Brazil kitategemea nini atafanya Uwanjani lakini alidokeza kuwa kuumia kwa Christian Benteke kumezidisha nafasi yake kucheza Kombe la Dunia.
Wilmots amesema: “Kwa hakika huyu ni Mchezaji wa kuvutia na hasa baada kukosekana Benteke. Watu wengi hawajui kuwa akiwa na Timu ya Rizevu ya Manchester United mara nyingi amecheza kama Namba 9. Kumudu kwake nafasi nyingi ni mali!”

Related Posts:

  • KAULI YA BALOTELI BAADA YA KUTUA RASMI LIVERPOOL "Nadhani nilifanya makosa kuondoka England,nilipenda kwenda Italy lakini nmegundua lile lilikua kosa" >Akizungumzia  huamisho wa Baloteli kocha wa Liverpool Brandan Rosgers amesema "Uhamisho huu umefata misingi ya kl… Read More
  • Barcelona yaanza ligi kwa ushindi mnono.. Barca imefungua msimu kwa ushindi mkubwa dhidi ya Elche Lionel Messi alifunga mabao mawili na kuisaidia Barcelona kuilaza Elche mabao 3-0 katika me… Read More
  • Kikosi cha taifa stars kitakachopambana na Morocco chatajwa. Morocco ( Atlas Lions) v Tanzania ( Taifa Stars), 5 Septemba... Haya ni majina ya wachezaji wa STARS yaliyotangazwa na mkufunzi mkuu, Martin Nooij.... MAKIPA, Deogratius Munish ( Yanga SC), Mwadini Ally Mwadini ( Azam FC),… Read More
  • SIMEONE AFUNGIWA MECHI NANE Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone amefungiwa mechi nane kwa utovu wa nidhamu alioonesha kwenye mechi ya Spanish Super Cup. Simeone, 44, alimgusa mmoja wa waamuzi kisogoni katika mechi iliyokuwa imejaa hamasa kati ya Atl… Read More
  • Manchester City yaigaraza Liverpool. MABINGWA wa England, Manchester City, Jana Usiku wakiwa kwenye uwanja wao Etihad wameonyesha kuwa hawana mzaha walipoitandika Timu iliyomaliza Nafasi ya Pili Msimu uliopita, Liverpool,magoli 3-1 katika Mechi ya Ligi Kuu … Read More

0 comments:

Post a Comment