Facebook

Tuesday, 29 April 2014

Waisilamu wautoroka mji wa Bangui tena



Hali ya taharuki imetanda mjini Bangui kutokana na vita vya wenyewe ka wenyewe
Walinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamewasindikiza zaidi ya waisilamu,1,200, kutoka katika mji mkuu wa CAR Bangui kutokana na tisho kwa usalama wao.
Waisilamu hao ni baadhi ya waisilamu waliosalia mjini Bangui ambao walilengwa kushambuliwa na wakristo katika mzozo wa wenyewe kwa wenyewe.

Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu waasi wa Seleka, kupindua serikali mwezi Machi mwaka jana.
Waasi hao wa Seleka walituhumiwa kwa kuwashambulia wakristo na kuchochea ghasia hizo zaidi. Gasia zilizozuka hata hivyo zilikuwa za kulipiza kisasi.


Sio mara ya kwanza kwa waisilamu kuondoka mjini Bangui
Pia kulikuwa na ripoti kwamba watu 22 wakiwemo machifu 15 na wafanyakazi wa shirika la Medecins Sans Frontieres (MSF), waliuawa mjini Nanga Boguila.
Mauaji hayo yalifanyika siku ya Jumamosi wengi wa waathiri wa wakiuawa wakati kliniki ya shirika hilo iliposhambuliwa.
Punde tu msafara huo ulipoondoka mjini Bangui, watu walivamia nyumba na majumba ya biashara yaliyokuwa yanamilikiwa na waisilamu hao na hata pia kuvamia msikiti.
"hatukuwataka waisilamu hapa na wala hatutaki msikiti wao,'' alisema mvamizi mmoja kwa jina Guy.
Waisilamu wachache sana wamebaki mjini Bangui lakini maelfu wametoroka katika siku za hivi karibuni, huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda.
Shirika la Amnesty International limetuhumu walinda amani kwa kukosa kuzuia mauaji ya halaiki.

Related Posts:

  • Shule UN yashambuliwa Palestina Uharibufu ulionywa Gaza na majeshi ya Israel Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa kutoka eneo la Gaza wamesema kuwa wana Shule ya Umoja wa Mataifa ambayo maelfu ya wapalestina walikuwa wameifanya kama makazi imepigwa na… Read More
  • Al Shabab yamuua Mwanamke kwa kutojifunga hijab Somalia. Wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab wamempiga mwanamke mmoja risasi na kumuua kwa kukosa kujifunga hijab kichwani. Jamaa za mwanamke huyo m… Read More
  • Mke wa mwanasiasa atekwa Cameroon Jeshi la Cameroon linasema kuwa kundi la wapiganaji Waislamu la Nigeria, Boko Haram, limemteka nyara mke wa mwanasiasa mashuhuri kaskazini mwa nchi. Mke wa naibu waziri mkuu, Amadou Ali, na msaidizi wake wa nyumban… Read More
  • Papa aomba vita vimalizwe Papa Francis ameomba amani kwa dhati katika hotuba ya kila juma katika medani ya St Peter's mjini Rome. Aliacha kusoma hotuba aliyoandika kuomba vita vimal… Read More
  • Ukrain kujibu mapigo Jeshi la Ukrain limeanza kujihami mashariki mwa nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya waasi wa Urusi kufuatia kutunguliwa kwa ndege ya Malaysia katika eneo hilo. Msemaji wa serikali ya Ukrain Andriy… Read More

0 comments:

Post a Comment