Facebook

Sunday, 27 April 2014

Van Gaal ambakisha RVP Man Utd..................


Photo


HALI shwari sasa!. Mshambuliaji wa Manchester United, Mholanzi, Robin Van Persie ameamua kuendelea kukaa katika klabu hiyo kufuatia kufukuzwa kwa David Moyes.
Kilichomvutia zaidi nyota huyo ni klabu hiyo ya Old Trafford kutaka kumleta Mholanzi mwenzake, Louis Van Gaal kurithi mikoba ya ukocha mkuu.
Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa Van Gaal tayari ameshakubali vipengele vya mkataba saa 48 zilizopita ili kuwa kocha wa kudumu wa Man united.
Sio siri kuwa Van Persie amekuwa na mahusiano mazuri na kocha wake wa timu ya taifa na sasa anaona itakuwa jambo zuri kukaa pamoja Old Trafford baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Taarifa za ndani ni kuwa kocha huyo wa Uholanzi na nahodha wake RVB wanatumia wakala mmoja, bwana Kees Vos ambaye kwasasa yupo katika vikao vya makubaliano ya kazi mpya baina ya Van Gaal na Man United.
Van Persie alikuwa akihusishwa kuihama Man United majira ya kiangazi mwaka huu kwasababu klabu yake imeshindwa kufanya vizuri kama ilivyokuwa katika msimu wake wa kwanza ambao alibeba taji chini ya Sir Alex Ferguson.
Pia kulikuwa na hali ya kutoelewa na bosi wake David Moyes kwa madai kuwa mbinu za ufundishaji za Mscotish huyo zilikuwa haziendani na mfumo wa uchezaji wa Van Persie.
Lakini nahodha huyo wa zamani wa Asernal ameamua kukaa Man United hata kama klabu inatarajia kusaka mshambuliaji mwingine wa kati kwa sababu bosi wake anakuja.

Related Posts:

  • Arsenal yamtengea dau Kondogbia.Hakuna timu ambayo ipo nyuma kupata wachezaji wazuri kwa ajili ya msimu ujao. Ukikaa nyuma muda wa usajili maisha hayatakua mazuri muda wa msimu ujao. Arsenal inakomaa kumpata mchezaji Kondogbia ambae pia anatakiwa na Inter m… Read More
  • Van Gaal amafungia kazi kiungo SchweinsteigerMchezaji nyota wa Bayern Munich Bastian Schweinsteiger anabaki chaguo namba moja la timu ya Manchester United kwa nafasi ya kiungo msimu huu.Lakini United wapo tayari kumpata mchezaji kiungo wa Southampton Morgan Schneide… Read More
  • Benitez atambulishwa rasmi Real Madrid.  Rafael Benitez ametambulishwa rasmi kama meneja mpya wa Real Madrid. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema: "Hii ni ngumu, kutakiwa kuzungumza, lakini sijui niseme nini," amesema meneja huyo wa zama… Read More
  • Gundogan atua Man UnitedManchester united imezipiku timu za Bayern Munich na Barcelona kwenye vita ya kupata saini ya mchezaji wa Borussia Dortmund. Mchezaji huyo ambae anacheza sehemu ya kiungo amekubaliana mambo ya msingi na Manchester united. Gun… Read More
  • Falcao akubali kutua Chelsea.Kama BantuTz tulivyo ripoti hapo mwanzoni kwamba mama yake Falcao alisema kwamba mwanae hana furaha ndani ya Manchester united. Kwa hiyo lazima alikua anatarajiwa kuondoka Old Trafford baada ya msimu kuisha. Habari ikufikie k… Read More

0 comments:

Post a Comment