Facebook

Sunday, 27 April 2014

Nissan watengeneza gari linalojiosha lenyewe..shuhudia hapa..................


Sasa naona Nissan wameamua kumvuruga kichwa mshkaji wangu Emmanuel Mchunguzi, na gari lao jipya lenye uwezo wa kujisafisha lenyewe, yaani hakuna kuosha gari kabisa.
 usishtuke sana bwana Emmanuel Mchunguzi, Nissan walaaaa, wanafanya yao tu, ila licha ya kuwa ni gari kali, lakini siwezi kuliita gari linalojiosha lenyewe (mtanisamehe Nissan) bali ni gari ninaloweza kusema halishiki uchafu wa aina yoyote, na hata hiki kipande cha video kilichotolewa na Nissan kinathibitisha hili.
Nissan wameanzisha rangi isiyoruhusu. vumbi, matope, uchafu wala maji kubaki kweye body ya gari na kuiacha gari ikiwa ina ng'ara bila ya kuiosha wala kuifuta.
 Kwa mujibu wa Nissan rangi hiyo inazuia maji na mafuta pia, na ubunifu huo ulifanikiwa kwa "kutengeneza tabaka la kinga ya hewa kati ya rangi na mazingira".


Rangi hiyo inaitwa Ultra-Ever Dry na imetengenezwa na UltraTech International Inc.







Gari hili la majaribio linaonyesha upande wa kulia uliopakwa rangi hiyo na upande wa kushoto wenye rangi ya kawaida.

Angalia video hiyo hapa chini...
 
 

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kufahamu maendelea ya kasi yanayofanyika katika nyanja ya sayansi natechnolojia

Related Posts:

  • Apple wazindua bidhaa mpya.Kampuni ya Apple imezindua saa ya kisasa - the Apple Watch - ambayo ni bidhaa yake mpya tangu iPad ya kwanza na tangu kifo cha mmoja wa waasisi wake Steve Jobs. Kifaa hicho huendesha programu tumishi (apps) na pia hufuatilia … Read More
  • Nyangumi apatikana Mtwara.Mzoga wa samaki aina ya nyangumi Umepatikana katika pwani ya Bahari ya Hindi Mkoani Mtwara na kisha kuvutwa Kuelekea majini na wavuvi wa Kata ya Msangamkuu. Mzoga huo una urefu wa futi 48 na uzito unaokadiriwa kuwa zaidi ya t… Read More
  • Matangazo tiba za asili yapigwa marufuku. Matangazo ya tiba za asili yanaelezwa kupotosha uma Baraza la Tiba za Asili na Tiba Mbadala Tanzania limesitisha vibali vya kurusha matangazo ya tiba za asili na mbadala kwenye vyombo vyote vya habari kwa kile kili… Read More
  • Wanafunzi 12,000 wakosa nafasi Vyuo vikuu,TCU yawapa nafasi ya Pili.Wanafunzi 12, 000 wakosa nafasi za vyuo vikuu, TCU yawapa nafasi ya pili kuchagua nafasi za masomo (course) ambazo bado ziko wazi na wameshauriwa kutochagua "course" zenye ushindani mwingi maana hii itasababisha wengine kukos… Read More
  • MIFUPA YA DINOSARIA "GODZILLA" YAPATIKANA TANZANIAAina mpya ya dinosaria imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania. Mabaki hayo ya dinosaria yaliyopewa jina la - Rukwatitan Bisepultus - yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa, kusini magharibi… Read More

0 comments:

Post a Comment