Facebook

Monday, 28 April 2014

Afrika Kusini huru yatimiza miaka 20...........

Afrika Kusini ikisherehekea kutimiza miaka 20 ya uhuru

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekuwa akiongoza sherehe za kutimiza miaka 20 ya demokrasi na kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi.
Akihutubia taifa Rais Zuma alisema Afrika Kusini inaanza kupona vidonda vya historia ya ukatili na mgawanyiko na taratibu inajenga umoja wa taifa.
Lakini alisema bado kuna kazi ya kukamilisha lengo la kuondosha umaskini, tofauti za pato na ukosefu wa ajira.
Sherehe hizo zinafanywa kabla ya uchaguzi mkuu ambapo chama tawala cha ANC kinakabili upinzani dhidi ya uongozi wa nchi tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka wa 1994

Related Posts:

  • Wagonjwa wa Ebola watoroka hospitalini Watu zaidi ya miatano tayari wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika kanda ya Afrika Magharibi Serikali ya Sierra Leone imeonya kuwa ni … Read More
  • Mlipuko waua watu 10 nchini Nigeria Takriban watu 10 wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika mji wa Bauchi Kaskazini mwa Nigeria. Kwa mujibu wa polisi, shambulizi hi… Read More
  • Alazwa hospitalini baada ya kumkana Mungu Mubarak Bala Mwanamume mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moj… Read More
  • Uingereza yaomba ruhusa ya jeshi lake Wanajeshi wa Uingereza Uingereza imesema kuwa inafanya mazungumzo na kenya ili kutatua mzozo kuhusu mafunzo ya wanajeshi wa Uingereza nchini humo. Serikali ya Kenya inaaminika kuchelewa kuwaruhusu wanajeshi zaidi wa … Read More
  • Wanajeshi wa Iraq wauteka mji wa Tiqrit Wanajeshi wa Iraq wakielekea mjini Tiqrit Serikali ya Iraq inasema kuwa vikosi vyake vimeuteka mji wa kazkazini wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji wa ki-sunni ambao walikuwa wameteka mji huo wiki mbili zilizopita. Vyo… Read More

0 comments:

Post a Comment