Sunday, 27 April 2014
Rais Kikwete:Muungano wetu ni mfano wa kuigwa bara la Afrika
Rais Jakaya Kikwete amesema Bara la Afrika lina jambo la kujifunza kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliodumu kwa miaka 50.
Amesema kuwa kitendo cha Muungano kudumu, kuimarika na kuendelea kustawi kwa nusu karne siyo jambo linaloweza kubezwa na nchi yoyote kwa kuwa zipo baadhi ya nchi zilizojaribu kufanya hivyo, zikashindwa.
“Wapo wenzetu barani Afrika walijaribu, lakini hawakufanikiwa kama sisi, kwani Muungano wao ulidumu muda mfupi na kusambaratika. Wapo waliokaa miaka miwili, miezi na wapo ambao wameanza majadiliano mpaka leo hawajamaliza,” alisema Kikwete.
Kikwete alisema hayo jana Dar es Salaam, wakati akipokea matembezi ya vijana na kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari.
Akinukuu maneno ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, Kikwete alisema: “Tanzania ni lulu ya pekee kabisa katika historia ya Afrika, nchi nyingine zote ni za kurithi kutoka ukoloni, Tanzani ni ya kuundwa na sisi wenyewe, kwa hiari yetu wenyewe baada ya kukomboa sehemu zake kutoka ukoloni.”
Alisema, mafanikio yaliyopatikana Tanzania yanaonyesha kuwa pia Shirikisho la Afrika Mashariki linaweza, na nchi za bara la Afrika kuungana na kuwa nchi moja inawezekana.
“Ikiwepo nia thabiti, mambo yakipangwa vizuri, hakuna kisichowezekana kwani njia itapatikana, sisi tumeweza na wenzetu pia wanaweza,” alisema.
Huku hotuba yake ikikatizwa mara kwa mara na vijana waliokuwa wakishangilia, Kikwete alisema kiini cha hotuba yake ni kutaka kujibu maswali mawili yanayohusu Muungano.
Aliyataja maswali hayo kuwa ni; kwani nini muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezekana na kwa nini umedumu.
Akijibu maswali hayo, alisema kuwa kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, asilimia 91 ya Watanzania walizaliwa baada ya Muungano na kwamba asilimia tisa tu, ndiyo waliozaliwa kabla ya Muungano huo.
Hivyo, aliamua kujenga hoja za majibu yake kwa kutaja mambo sita aliyoyataja kuwa ndiyo siri ya mafanikio ya Muungano.
Mambo hayo ni kwamba waasisi wa Muungano, Nyerere na Abeid Karume, walikuwa na nia ya dhati ya kuungana, walitanguliza maslahi ya taifa mbele na kuwa watu wa Tanganyika na Zanzibar ni wamoja.
Mambo mengine ni kuwepo kwa uhusiano wa karibu kati ya viongozi wa kisiasa wa Tanganyika na Zanzibar, nia ya kutatua matatizo yanayohusu Muungano na kwamba Muungano unawanufaisha watu, vinginevyo ungekuwa umeshakufa zamani.
Lugha za matusi bungeni
Kikwete alisema kuwa amesikitishwa na matumizi ya lugha za matusi na vijembe zilizotumiwa na Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, hata baada ya kuwazuia kufanya hivyo wakati akizundua Bunge hilo.
“Inaelekea ushauri wangu hawakuuzingatia, wanatumia lugha za matusi yanayokaribia kuwa ya nguoni,” alisema.
Pia, aliwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba wa Wananchi (Ukawa) kurejea bungeni kwa kuwa wananchi hawatawasaidia kutatua matatizo yao, badala yake watasikitika nao tu.
Alisema kuwa hakufurahishwa hata kidogo na kitendo cha Ukawa kutoka nje ya Bunge kwa kuwa anaamini suluhisho lao linapatikana ndani ya Bunge.
Vijana zaidi ya 3,000 kutoka mikoa mbalimbali nchini na maeneo tofauti jijini Dar es Salaam jana walikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria katika ukumbi wa PTA, kusikiliza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya maadhimisho ya dhahabu ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Huku wakiwa wamevaa fulana nyeusi zilizokuwa na ujumbe uliosomeka ‘2 zinatosha’, ukimaanisha muundo wa Serikali mbili unaoungwa mkono na CCM
Related Posts:
"TWEETS" ZA WATU MASHUHURI NA TAASISI MBALIMBALI KUHUSIANA NA SAKATA LA ESCROW. BantuTz.com @BantuTz Mwenyekiti wa Bunge ametumia madaraka yake kuahirisha Bunge mpaka saa kumi na moja jioni. Ripoti ya Zitto(PAC) haikuanza kujadiliwa … Read More
LIVE !!! KUTOKA BUNGENI DODOMA:-UWASILISHWAJI WA RIPOTI YA PAC KUHUSU TEGETA ESCROW ACCOUNT.SAA 11:25 JIONI Baada ya bunge kwenye kikao cha asubuhi kusema swala la Escrow limeingizwa kwenye ratiba na ripoti itawasilishwa kuanzia jioni ya leo. Tujumuike kwa pamoja kuhabarishana yanayojiri jioni hii bungeni Dodoma … Read More
LIVE FROM DODOMA-SAKATA LA ESCROW5:3O ASUBUHI BUNGE LIMEHAIRISHWA MPAKA SAA 11:00 JIONI Mh Kafulila kazungukwa na wabunge wengi sana nje wanampongeza kwa kuoa. 5:25 ASUBUHI MIONGOZO (Nchambi): Kuna taarifa mahakama imepinga kujadili Escrow (anazo… Read More
BantuTz MAGAZINE-Soma kilichoandikwa katika Magazeti ya leo Novemba 27. BantuTz MAGAZETI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa… Read More
SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC ILIYOSOMWA SASA BUNGENI HIVI PUNDE.Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe. Andrew Chenge (Mb) Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6. Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 6… Read More
0 comments:
Post a Comment