Monday, 28 April 2014
Sababu kamili ya P-Funk kufunga ndoa ya siri hii hapa.............
Baada ya kuishi maisha ya kisela kwa muda mrefu, hatimaye mtayarishaji nguli wa muziki Bongo, Paul Mathyasse ‘P Funk’ ameoa kwa siri.
Mtayarishaji nguli wa muziki Bongo, Paul Mathyasse ‘P Funk’ wakati wa harusi yake. Taarifa kutoka kwa chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo, lilichukua nafasi jijini Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita kwa usiri mkubwa. Imeelezwa kuwa, P Funk aliamua kumuoa rasmi mzazi mwenzake, Samira baada ya kuishi naye kwa miaka kadhaa kama mke na mume lakini haikujulikana mara moja sababu za kuweka usiri katika tukio hilo la kheri.
Maharusi wakipongezwa na ndugu na jamaa zao baada ya ndoa. “Jamaa (P Funk) amevuta jiko rasmi kwa siri kubwa lakini ameamua kufanya siri hata sijui ni kwa nini, tukio limechukua nafasi huku Arusha na watu kadhaa walialikwa lakini mastaa siyo wengi. “Sherehe imefana, watu wamekula, wamekunywa kwelikweli maana misosi ilikuwepo ya kumwaga,” kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, katika harusi hiyo, kulikuwepo na ulinzi mkali wa watu kuzuiwa kupiga picha hivyo matukio mengi kushindwa kusambaa mtandaoni. “Daah! Ilikuwa ngumu sana, watu hawakuruhusiwa kupiga picha, hata simu zilizotumika zilikuwa zaidi ni za bwana na bibi harusi na ndugu wa karibu,” kilisema chanzo.
Mke wa P Funky. Paparazi wetu aliposhibishwa habari hizo na baadhi ya picha kuvuja katika Mtandao wa Instagram, alimvuti waya P Funk lakini simu yake ya kiganjani iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Related Posts:
Safari ya Uturuki yataka kumuua Mzee Mjuto MSANII wa maigizo na filamu nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ ameeleza kuwa, kwa furaha aliyonayo baada ya kupata safari ya kwenda Uturuki imemfanya ajisikie kufa kwani ni bahati ambayo hakuitarajia.zee Majuto a… Read More
Yaliyojiri kwenye Birthday Dinner Party ya MBONI MASIMBA Yaliyojiri kwenye birthday dinner party ya MBONIE MASIMBA (@thembonishow) pale RHAPSODY’S VIVA TOWER Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata habari mbalimbali zinazowa… Read More
Picha,Mtindo Mpya Wa Nywele Wa Mike Sonko Katika Kumpa Ushirikiano Rais Uhuru Kenyatta. Tunapozungumzia fashion ya mwanasiasa au kiongozi wa raia sehemu yeyote duniani mara nyingi tunatazama mavazi na muonekano wa heshima mbele za watu. Kwa Seneta wa Nairobi Mike Sonko hio ameweza kufanya na kuongeza swaga … Read More
Picha Za Diamond na Ommy Dimpoz London....... Diamond alikwenda Uingereza kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake na Iyanya ambayo imegharimu zaidi ya dola za kimarekani elfu 20 (zaidi ya milioni 30 za Tanzania) kutokana na ukubwa wa director wenyewe, … Read More
Wema, Diamond Wachafua Hali ya Hewa JAMBO limezua jambo. Pamoja na kuanza kwa kishindo safari yake ya kuelekea Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa ajili ya fainali za kuwania Tuzo za MTV Africa (MAMA), mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na baby wake, Wema … Read More
0 comments:
Post a Comment