Facebook

Monday, 28 April 2014

Tanzania yaichapa Kenya 4-3................




Timu ya taifa ya soka ya Tanzania kwa vijana wenye umri wa miaka 20 imesonga mbele kwenye safari ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la mataifa baada ya kuilaza Kenya kwa mikwaju ya Penalti 4-3 kwenye mechi ya marudiano iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo imelazimika kuingia hatua ya Penalti baada ya kumalizika dakika 90 mechi ikiwa sare ya 0-0 na ndipo Tanzania ilipopata ushindi unaoisogeza kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo inayofanyika kila baada ya miaka miwili.
Ushindi huo wa timu ya Tanzania ijulikanayo kana Ngorongoro Heroes umekuwa faraja kwa Watanzania baada ya timu ya Taifa ya wakubwa, Taifa Stars kuchezea kichapo dhidi ya Intamba Murugamba ya Burundi Jumamosi kwenye mechi ya kirafiki ya maadhimisho ya miaka hamsini ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa mabao 3-0.
Nalo Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limemtangaza rasmi kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Martinus Ignatius Nooij ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuionoa timu hiyo huku kibarua chake cha kwanza kikiwa tayari kimeishatangazwa ambapo Taifa Stars itashuka dimbani dhidi ya Zimbabwe mwezi Mei mwaka huu kwa mechi ya awali ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa zitakazofanyika mwakani nchini Morocco mwezi Februari mwakani.
Tayari Kocha ametangaza majina ya wachezaji tisa wapya kuimarisha kikosi hicho huku beki maarufu wa timu ya Yanga, Kelvin Yondan akitemwa kwenye kikosi hicho baada ya kugoma kuripoti kambini, pasipo kutoa sababu za msingi za kutofanya hivyo.
Katika safari ya kuelekea Morocco hapo mwakani, Uganda itashuka dhimbani dhidi ya Madagascar,huku Burundi ikicheza dhidi ya Botswana,na Harambee Stars ya Kenya itapepetana na Commoro,nayo Rwanda ikicheza dhidi ya Libya.

Related Posts:

  • Ulaya wataka Blatter ajiuzulu kwa usemi Rais wa Shirikisho la kandanda duniani, FIFA, Sepp Blatter. Maafisa wa kandanda wa Europa sasa wamemtaka rais wa shirikisho la kimataifa… Read More
  • Brazil 3-1 Croatia 00:55 Mechi imekamilika . Brazil 3-1 Croatia . 00:54 Mechi hii imekamilika Brazil ikisajili ushindi mkubwa wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia. … Read More
  • Matumaini ya Brazil yako kwa Neymar Pele; Neymar asiachiwe mzigo pekee yake Mchezaji wa kitambo wa Brazil ana wasiwasi kuwa taifa hilo linamshinikiza mshambulizi wa Neymar kuisaidia taifa hilo kunyakua taji la Kombe la Dunia kwa wenyeji hao na huen… Read More
  • Wadhamini wa kombe la Dunia taabani. Hadhi ya makampuni yanayothamini kombe la Dunia taabani Brazil. Udhamini wa kandanda duniani umekua kwa kiasi kikubwa na sasa unazidi utoaji wa fedha kwa mashirika yanayoisimamia kwa shirika la soka duniani Fifa.Ki… Read More
  • Maajabu ya mmiliki wa klabu ya Southampton.. Katharina Liebherr: Jina hili la mama huyu kibonge si maarafu sana katika vichwa na midomo ya wapenda soka duniani hasa bongo,labda ni kwa sababu ya jinsia yake ama ni kutokana na tabia yake ya kujiweka mbali na vyomb… Read More

0 comments:

Post a Comment