Facebook

Sunday, 20 April 2014

Taulo la Ivo lazua kizaa zaa taifa, lahusishwa na Uchawi laleta ugomvi Simba na Yanga.......soma hapa............!!!


 
    Katika mchezo wa Simba na Yanga Leo Ambao wametoka droo kwa kufungana goli moja kwa moja palitokea kituko ambacho kimewaacha wengi huo...Kama Kawaida yake Ivo Mapunda akiwa langoni Huwa anakuwa na Taulo kubwa Jeupe la kujifutia Jasho Ambalo hulininginiza Kwenye Nyavu za Goli ..Leo Mchezaji Didier Kavumbagu Baada ya Yanga kukosa Goli langoni Hapo aliamua kulichukua Taulo hilo na Kukimbia Nalo na kulitupa kwa Mashabiki ...Kwa kile kinachodaiwa ni Dumba inayozuia Yanga Wasifunge....Ilibidi mchezo usimame kwa muda baada ya kuanza kushikana mashati kuhusu hilo taulo, Mwishowe Taulo lilirudi kwa Ivo Mapunda na Mchezo Kuendelea....

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbali mbali za michezo

0 comments:

Post a Comment