Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Thursday, 17 September 2015

Taarifa ya NCCR-MAGEUZI kwa Vyombo vya habari kuhusian na UKAWA.

NCCR – MAGEUZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI,
DAR ES SALAAM, ALHAMISI, 17 SEPTEMBA 2015
USHIRIKI WA VYAMA VYA NCCR – MAGEUZI, NLD, CUF NA CHADEMA KATIKA UKAWA.

UTANGULIZI
Sisi viongozi wa ngazi ya juu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu tukiwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa na viongozi wengine, tumekuja mbele yenu mtusaidie kufikisha ujumbe maalum kwa wanachama wetu na Watanzania wote wanaokiamini chama chetu,
Tumefika kuelezea kutoridhishwa na mwenendo wa ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA. Tumekuja pia kuwaelezea ni hatua gani tulizoamua kuchukua kukabiliana na changamoto hii.
Wengi wenu mnafahamu kuwa UKAWA ni Umoja wa Katiba ya Wananchi ulionzishwa wakati wa Bunge Maalum la Katiba kutetea Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi dhidi ya uchakachuaji uliokuwa unafanywa na CCM.

UKAWA  siyo chama cha siasa bali umoja. NCCR-Mageuzi iliamua kujiunga na harakati hizi kwa nia njema ya kutetea maslahi ya taifa letu. Zaidi ya mwaka sasa tangu tujiunge na umoja huu, matokeo yake yamekuwa ni mabaya kwa uhai na ustawi wa chama chetu. Wakati vyama vingine vimezidi kuimarika ndani ya UKAWA, NCCR-Mageuzi imedhoofika. Hali hii haikubaliki.
MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO BAINA YA VYAMA VYA UKAWA
Vyama vinavyounda UKAWA, vilisaini Makubaliano ya Ushirikiano katika Mkutano wa Hadhara kwenye viwanja vya Jangwani. Kitendo hicho kiliwavutia na kuwapa matumaini wananchi na wao wakazidi kutuunga mkono. Iliamuliwa kwamba tusiuwe vyama vyetu bali tuunganishe nguvu za vyama vyetu kama namna ya kujiimarisha kwa pamoja.
UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA DISEMBA 2014.
Kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2014, vyama vinavyounda UKAWA vilitiliana saini ya Mwongozo wa Ushirikiano katika Uchaguzi huo.
Licha ya kutiliana saini Makubaliano hayo, bado kulikuwa na ukiukwaji mkubwa na wa makusudi  wa Mwongozo huo.
Licha ya kuzijadili changamoto zilizojitokeza katika Uchaguzi huo, lakini hazikupatiwa ufumbuzi wowote.
Sisi tuliopo hapa tulionya mapema kuhusu mwenendo huu wa kuvunja makubaliano na tukaomba taratibu tulizokubaliana zitumike ili kurudi kwenye misingi ya UKAWA lakini hatukusikilizwa.

USHIRIKIANO KATIKA UCHAGUZI MKUU, OKTOBA 2015.
Licha ya changamoto zilizokuwepo, tuliamua kwa pamoja kwamba vyama vya UKAWA tuingie katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na makubaliano ya ushirikiano, ikiwemo kuwa na mgombea mmoja wa Urais na kuachiana majimbo ya uchaguzi.
Pia, katika kuendesha umoja huu, tuliunda vyombo vya kutusaidia ambavyo ni:-
Kamati ya Wenyeviti.
Kamati ya Makatibu Wakuu.
Kamati ya Ufundi.
Kamati ya Wataalam.
Pamoja na kuunda vyombo vya kuendesha UKAWA, tangu Januari 2015, bado tumeshindwa kujenga UKAWA imara na tuliyotarajia kwa manufaa ya wanaukawa  na wananchi kwa ujumla.
Yafuatayo yamethibitisha hili jambo:
Tumeshindwa kuweka Kanuni za uendeshaji wa UKAWA kama tulivyokubaliana. Kwa maana hiyo, tunafanya mambo kiholela
Tumeshindwa kuunda Kamati zitakazoshughulikia migogoro baina ya vyama.
Tumeshindwa kuunda na kuzisimamia Kamati za Majimbo
Tumeshindwa kupata muafaka wa kuachiana majimbo.
Mfano, NCCR – Mageuzi tuliachiwa majimbo 12 ya Kasulu Vijijini, Kigoma Kusini, Muhambwe, Kasulu Mjini, Vunjo, Ileje, Mbinga Mjini, Manyovu, Buyungu, Ngara, Nkenge na Korogwe mjini. Ikumbukwe kwamba, mwaka 2010, NCCR-Mageuzi ilisimamisha wagombea katika majimbo 67.
Kwa maana hiyo, UKAWA umeturidisha nyuma katika kupata wabunge na kuimarisha chama zaidi ya miaka 20 baada ya kuundwa kwake.

Licha ya kukubaliana kwamba NCCR-Mageuzi iachiwe majimbo 12, wenzetu wa vyama vingine katika UKAWA wamesimamisha wagombea katika majimbo 6 kati ya hayo. Wametuvunja moyo na kutuonyesha kwamba hawatujali. Na hata kule ambapo katika majimbo sita ambapo wametuachia bado wenzetu wanatufanyia fujo kuliko hata wanazotufanyia wanachama wa CCM. Tunamifano mingi ya kuonyesha ni jinsi gani wagombea wetu wanavyofanyiwa vurugu. 

Tumeshindwa kupata muafaka wa namna ya kuachiana wagombea udiwani katika kata nyingi.
Tumeshindwa kuonesha na kukubaliana kila chama kitapata nafasi gani na ngapi katika Serikali ya UKAWA.
Tumeshindwa kufuata utaratibu wa kumpata mgombea Urais wa UKAWA
Tumeshuhudia vurugu kubwa iliyoletwa ndani ya UKAWA na wanachama waliotoka CCM na wao kupewa umuhimu kuliko viongozi wa UKAWA. Zaidi ya Mbatia hakuna kiongozi wa NCCR-Mageuzi anayeshirikishwa, anayezungumza au aliyepo kwenye kampeni za mgombea Urais wa UKAWA.
Tumeshindwa kuwa na timu ya kampeni timu ya UKAWA, ambayo inagharamiwa na UKAWA na inatafuta fedha pamoja, kama ilivyokubaliwa.
Tunashuhudia UKAWA ambayo Chadema ndiyo UKAWA-Bara na CUF ndio UKAWA-Zanzibar. Chadema haijali Zanzibar na CUF haijali Bara. Na NCCR-Mageuzi haipo huku wala kule ikiendelea kudhoofika siku hadi siku. 
Tumeshindwa kuona uwazi katika matumizi ya fedha na maamuzi muhimu ya uendeshaji wa UKAWA.
Tumefadhaishwa na kuvunjwa kwa misingi ya kuanzisha kwa UKAWA.
Wakati NCCR imetii mgawanyo wa majimbo kwa vyama vinavyounda UKAWA, vyama vingine na hasa CHADEMA vimesimamisha wagombea kinyume cha makubaliano.

NINI KIFANYIKE NA UKAWA

Hatukuwaita hapa kuwaambia kwamba tunajiuzulu siasa kutokana na changamoto hizi. Tumeamua kupambana na kurudisha hadhi na heshima ya Chama chetu. Hatuwezi kubwaga manyanga. Tunataka kuitoa CCM madarakani kutokana na ulaghai na ujanja-ujanja wa miaka 50. Lakini hatuwezi kuitoa CCM kwa mbinu za ulaghai na ujanja-ujanja. Tunakwenda kukabidhiwa dhamana ya kuongoza nchi na Watanzania. Tunao wajibu wa kujiongoza vizuri ili tuwaonyeshe Watanzania kwamba tuna uwezo wa kuwaongoza vizuri.




WITO WETU
Tunamshauri Mwenyekiti wetu, ndg. James Mbatia, aitishe vikao vya kikatiba ili tuweze kujadiliana kuhusu hatima ya chama chetu.
Tunashauri ndg. Mbatia asiwemsemaji wa CHADEMA wakati anakiacha chama chake (NCCR-Mageuzi)kinadhoofika. Kwa mfano, Dr. Slaa alipoishambulia Chadema hakuna kiongozi wa Chadema aliyemjibu isipokuwa Mbatia ndiye aliyeamua kujiingiza kwenye ugomvi ndani ya Chadema.
Tutachangishana ili tusafiri kwenye majimbo na kata za wagombea wetu na kuwasaidia kwenye kampeni ili wasibaki wapweke kama yatima.

Tunasisitiza kwamba upinzani wa kweli nchini hauwezi kujengwa kwa njia za hila, kwa kukiuka taratibu za kidemokrasia tulizojiwekea wenyewe, kwa kukiuka misingi muhimu kama uadilifu, kwa kuweka mbele tamaa na maslahi binafsi kuliko taifa, kwa kutegemea propaganda. Tukifanya hivi, wananchi watashindwa kututoufautisha na CCM na wataamua kuchagua zimwi walijualo. Hatari hii tunaiona wazi kabisa.

……………………………
Leticia Ghati Mossore                       
                        Makamu Mwenyekiti (Bara)
NCCR-Mageuzi
17.09.2015

Mosena Nyambabe
Katibu Mkuu, NCCR Mageuzi

Bondia afariki baada ya kupigwa kwa "Knock-Out"

Mwana masumbwi mmoja wa Australia amefariki siku nne baada ya kupoteza fahamu alipopigwa 'knock out' katika pigano la kijimbo mjini Sidney.

Davey Browne mwenye umri wa miaka 28 aliangushwa na Carlo Magali wa taifa la Ufilipino mwisho wa raundi ya 12 katika taji la uzani wa Feather siku ya Ijumaa.

Brown ambaye ni baba ya watoto wawili alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya mitambo inayomsadia kuzimwa alipokosa kuimarika kiafya.

Muungano wa wahudumu wa matibabu nchini Australia umetaka mchezo wa ndondi kupigwa marufuku nchini humo kufuatia kifo hicho.

Kifo cha Browne kinajiri wiki sita baada ya mwanamasumbwi wa Queensland Braydon Smith kuzirai na kufariki kufuatia pigano la uzani wa Feather nyumbani kwake huko Toowoomba.

Mourinho "Nilisahau utamu wa ushindi"

Kocha mkuu wa Chelsea Jose Mourinho amesema alikuwa amesahau utamu wa ushindi akizungumza baada ya vijana wake kujikwamua na kupata ushindi wa 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv.

Hii ni baada ya klabu hiyo kuanza vibaya ligi ya Premier ikishinda mechi moja pekee kati ya tano ilizocheza.

"Nilikuwa nimesahau mtu anavyohisi. Kwa muda mrefu hatukushinda mechi, inahisi vyema sana, ni hisia nzuri,” alisema Mourinho.

“Mimi huwa meneja mzuri ninaposhinda mechi na husalia meneja mzuri ninaposhindwa.”

Licha ya kuanza kwa mkosi wa Eden Hazard kupoteza penalti, mabao ya Willian, Oscar, Diego Costa na Cesc Fabregas yaliwawezesha Chelsea kuwalemea wapinzani hao kutoka Israel mechi yao ya kwanza Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya msimu huu.

"Penalti tuliyopoteza ilikuwa mtihani mkubwa sana kwetu,” Mourinho akaongeza. “Unapoanza mechi ambayo unahitajika sana kushinda na baada ya dakika tano unapoteza mechi, ni kisa cha kuvunja moyo lakini tulijibu vyema.”

Mourinho alikuwa ameangaziwa sana kabla ya mechi hiyo baada ya kilabu yake kuanza ligi vibaya zaidi tangu 1986.
Licha ya hayo, mashabiki waliohudhuria mechi hiyo ya Ulaya uwanjani Stamford Bridge bado waliimba na kumsfu jina lake lilipotajwa kabla ya mechi kuanza na walimuunga mkono mechi yote.

Akiongea baadaye, Mourinho alisema anafurahia mashabiki wanapomuunga mkono badala ya wanapoimba ‘Mourinho aendelee’

“Hili linaonyesha hawasomi magazeti au hawasahau haraka. Iwapo hawasomi magazeti, wananiunga mkono. Iwapo hawasahau upesi, wananiunga mkono,” akasema.

"Tulishinda mataji manne la Ligi ya Premier, matatu tukiwa naye na moja na timu yake. Huyu si jamaa mbaya. Tuunge mkono jamaa huyu. Tuna nafasi ya kushinda taji la tano,” akaongeza Mourinho, akiashiria yaliyo akilini mwa mashabiki wanaoendelea kumuunga mkono.

Chelsea ilikuwa ndiyo kilabu ya pekee kutoka Uingereza kushinda mechi za kwanza Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya baada ya Arsenal kulazwa 2-1 na Dinamo Zagreb na kujiunga na Manchester United na Manchester City katika kujikwaa.

Mourinho hata hivyo alisema angelipendelea kilabu hizo zishindwe mechi za ligi ya Premier badala ya Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya.

Endelea kutembelea www.bantuz kwa habari za kina na uhakika.

Hawa ndio wachezaji waliochaguliwa katika timu bora ya wiki hii katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Hawa ndio wachezaji waliochaguliwa katika timu bora ya wiki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

1.Gianluigi Buffon
2.Alessandro Florenzi
3.Diego Godin
4.Kostas Manolas
5.Angel Di Maria
6.Thiago Alcantara
7.Hakan Calhanoglu
8.Hulk
8.Thomas Muller
10.Vincent Aboubakar
11.Cristiano

Timu zilizoshinda Mechi nyingi Ligi ya Mabingwa barani Ulaya:
Real Madrid (125 wins)
Barça (119)
Manchester United na Bayern (107)

Maafisa wa kikosi cha ulinzi cha rais nchini Burkina Faso wametangaza kuvunja serikali ya mpito.

Maafisa wa kikosi cha ulinzi cha rais nchini Burkina Faso wametangaza kuvunja serikali ya mpito. Badala yake "Baraza la Kidemokrasia na Kitaifa" ndio litachukua udhibiti na kumaliza "utawala dhalimu", amesema afisa mmoja kupitia kituo cha TV cha taifa. Spika wa bunge wa kipindi cha mpito Cheriff Sy amesema hatua hiyo ni "mapinduzi dhahiri".

Kuna mapigano makali yanaendelea katika medani ya mapinduzi jijini humo. Siku ya Jumatano, kikosi cha rais kiliwakamata rais wa mpito na waziri mkuu. Walikuwa wakitarajiwa kukabidhi madaraka kwa serikali mpya Oktoba 11 baada ya uchaguzi. Rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu Blaise Compaore, aliondolewa madarakani mwaka jana kutokana na nguvu ya wananchi.

Viongozi NCCR MAGEUZI wajitokeza kuelezea kutoridhishwa kwao na mwenendo wa UKAWA

Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Mosena  Nyambabe azungumza juu ya Chadema kuteka Umoja wa UKAWA na kufanya ubabe katika katika upataji wa majimbo na kuacha vyama vingine vilivyo katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo katika Hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam hivi sasa.

Hatua waliochukua wamesema hawatajiuzulu lakini wanasema wataendelea kupambana ndani ya NCCR-MAGEUZI na katika umoja huo watapambana bila UKAWA.

Viongozi  waandamizi wa NCCR Mageuzi waliokuwa katika mkutano huo ni Bi Leticia Mosore (Makamu Mwenyekiti NCCR Mageuzi –Taifa), Ndugu  Mosena Nyambabe (Katibu Mkuu NCCR Mageuzi – Taifa) na Wajumbe mbalimbali wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya NCCR Mageuzi  cha NCCR Mageuzi  

Hoja kubwa katika mkutano huo ni:-

1.Kushindwa kukubaliana katika mambo mbalimbali waliokwisha kubaliana.

2.Kushindwa kufuata kwa taratibu ya kumpata mgombea wa ukawa.

3. Hakuna kiongozi wa NCCR MAGEUZI tofauti NA Mbatia anayeshilikishwa wala kusikilizwa katika kampeni.

4.Chadema ni UKAWA BARA NA CUF ni UKAWA ZANZIBAR

Endelea kufuatilia kila kitakachokuwa kinajiri kupitia www.bantuz.com

AYO'S MATA MAESTRO:- TIMU ZA UINGEREZA NA BALAA LA MASHINDANO YA KLABU BINGWA ULAYA

NINACHOKIAMINI MAESTRO.

TIMU ZA UINGEREZA NA BALAA LA MASHINDANO YA KLABU BINGWA ULAYA.

Miaka kadhaa nyuma timu za Uingereza zilisha kasi kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya. Lakini hivi sasa imekuwa kinyume chake. Kwa nini timu za Uingereza zimekuwa nyepesi sana kwenye mashindano hayo Ulaya!!?

VIWANGO,WACHEZAJI NA FEDHA.

Viwango vya timu za Uingereza kwa miaka hii ya karibuni havijatofautiana sana. Imekuwa ni jambo la kawaida timu za daraja la chini au za kiwango cha kawaida kuzifunga au kuzisumbua timu zenye viwango vya juu. Hii ni kutokana na miaka ya sasa kila timu ina uwezo wa kupata fedha na kununua wachezaji wanaowataka. Zamani timu kama Manchester United,Liverpool,Arsenal nk ndio zilikuwa na uwezo wa kutamba kifedha lakini sasa wadhamini ni wengi na wanawekeza popote pale kwenye masilahi,hasa mchezo wa soka umekuwa ni biashara kubwa sana kwa miaka ya sasa.

WAPINZANI NA VIWANGO VYAO:

Mashindano ya Ulaya huwa inazikutanisha timu nyingi sana kutoka ligi mbalimbali kutoka kwenye bara hilo. Wachezaji wengi wa sasa wa timu za Uingereza wana viwango vya kawaida kulinganisha na wapinzani wanao kwenda kukutana nao. Mfano ni timu zote ambazo zinawakilisha Uingereza kwenye mashindano ya Ulaya wachezaji wake hawakaribiani hata kidogo kwa uwezo na wachezaji wa timu wanazokutana nazo. Timu hizo sasa wanawategemea wakina  Martial,Depay,Herrera,Smalling,McNair,Conquelin,Berlin,Sterling,Bony,Paulista nk ndio wakapambane na timu zenye Lewandowski,Messi,Neymar, Suarez,Chiellini,Vidal, nk . Kama Newcastle, Crystal Palace,West Ham zinawasumbua vilivyo timu tegemezi inawezekana vipi timu hizo zikatoka salama nje ya nyumbani  kwao ambako kuna wakina Bayern Munich,Barcelona, Real Madrid,Atletico Madrid,PSG nk wenye wachezaji wa viwango vya ubora wa juu!!?

Wachezaji wa zamani wa timu za Uingereza hawakaribiani wala kulingana kwa viwango na wachezaji wa sasa wa timu hizo. Kama maisha yataendelea kuwa hivyo kwa timu za Uingereza itakuwa ngumu sana kwa timu hizo kupata mafanikio na heshima nje ya ardhi yao.

IMEANDALIWA: Ayo's Mata Maestro

Jengo refu Afrika lazinduliwa Tanzania.


Jengo la PSPF Towers lililozinduliwa na Rais Kikwete hapo jana ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi LILILOKAMILIKA Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa mita 147. Ujenzi wake ulitumia miaka minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 na limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Tanzania. Lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili kuna sehemu ya Mgahawa, Mabenki, Bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi, Maegesho ya Magari na sehemu nyingine muhimu.