Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Thursday, 12 November 2015

Dkt Slaa atoa tathmini ya maamuzi anayofanya Rais Dkt Magufili.

Aliyekuwa katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa ametoa tathmini yake kwa siku chache za Rais John Magufuli alizoanza kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano na maamuzi aliyoyafanya. 

Dkt. Slaa ambaye alikuwa mgombea urais kupitia Chadema mwaka 2010, ameeleza kuwa maamuzi ya kufuta safari za nje kwa watendaji wa serikali yaliwahi kuchukuliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere. 

Alisema kuwa hata wapinzani walikuwa wakilalamikia gharama zinazotumika kwenye safari za nje na kwamba yeye pia aliwahi kupendekeza safari hizo kufutwa na badala yake watendaji waende vijijini kuchagiza maendeleo. 

“Tulilamikia safari za Rais Mstaafu Jakaya Kikwete nje ya nchi. Na mimi niliwahi kusema kuwa tufute safari za njena kuanza kwenda zaidi vijijini.Ni siku mbili (Jumamosi) ofisini huwezi kufanya tathmini ya maana sana,” alisema. 

“Tathmini hii kwa kawaida hufanywa baada ya siku 100. Mwalimu alifanya hivyo. Rais wa watu ni vyema akifanya hivyo. Ndiyo namna pekee ya kujua hali halisi. Kwa Magufuli si ya kwanza, amefanya sana akiwa Waziri.”

Endelea kutembelea www.bantuz.com.

Sepp Blatter alazwa baada ya mshutuko.

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, Sepp Blatter amelazwa hospitalini kutokana na kupatwa mshituko wa neva.

Blatter aliyesimamishwa kwa siku 90 kujishughulisha na masuala ya soka wakati akichunguzwa kwa kashfa za rushwa , alilazwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa afya lakini sasa imeelezwa ataendelea kubaki huko.

Mwanamichezo huyo aliyeongoza ulimwengu wa soka kwa miaka 18 mpaka sasa, awali ilidaiwa alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo hivyo ikabidi apate huduma ya matabibu, sasa imebainika ana tatizo la mshituko wa neva.

Awali, mwanasheria wake, Richard Cullen alieleza juu ya uangalizi huo wa madaktari kutarajiwa, lakini akasema alitarajia arejee nyumbani mapema kabla hali kubadilika na kutolewa maelezo tofauti.

Hata hivyo, watu wake wa karibu wameeleza hali yake si mbaya na anatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida japokuwa atabaki hospitalini hadi mapema wiki ijayo.

Msaidizi wake, Walter Gagg, amesema kwamba bosi huyo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa hafla ya kukabidhi tuzo ya Mwanasoka Bora hapo Januari 11 mwakani.

Viti Maalum: BAWACHA Ruvuma wampa Mh. Mbowe siku 3.

BAWACHA Mkoani Ruvuma wampa Mwenyekiti Mbowe siku tatu kutengua uamuzi wa kumteua Zubeda Sakuru Ubunge Viti Maalum, wasikitishwa na uteuzi huo wadai ni wa upendeleo-Aidha wameshangazwa na uongozi wa Chama kutotokea kwenye kikao maalum cha kupinga uamuzi huo.

Wamesema wamesikitishwa kwa chama kuonyesha waziwazi kwamba ni mali ya mtu mmoja na familia yake.Iweje leo waletewe Mbunge wa Viti Maalum kutoka Tanga, hali hajui Mkoa wa Ruvuma ukoje na Jiografia yake. Aidha pia wameshangazwa na uongozi wa Chama hiko kutotokea kwenye kikao maalum cha kupinga uamuzi huo.

Rais Dkt Magufuli apokea hati ya makabidhiano ya Ofisi ya Ikulu kutoka kwa Rais Mstaafu Dkt Kikwete leo

Picha:-Rais Dk MagufuliJP akipokea hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu Dk J M. Kikwete Ikulu Dar leo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya apiga marufuku matumizi ya simu za mkononi wakati wa kazi

Mkuu wa mkoa wa Mbeya amepiga marufuku matumizi ya simu za mkononi wakati wa kazi mkoani Mbeya ili watumishi wa serikali na mashirika ya umma wahudumie jamii kwa wakati. 

Asisitizia marufuku mtandao wa WhatsApp, ataka watumishi wa Umma na Serikali wahudumie jamii kwa wakati zaidi.

Suleiman Matola aachia ngazi Simba SC.

Kocha msaidizi wa simba Suleiman Abdallah Matola amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na kile alichodai kutolelewana na Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan Kerr.

Matola amesema kwamba amefikia uamuzi huo baada ya kuona maelewano na bosi wake huyo yanazidi kuwa magumu kila kukicha."Ni jambo la muda mrefu, huyu kocha hasikilizi ushauri wangu, imefikia sasa ananichukia na kazi haziendi tena.

Sasa nimeona ili kuepusha matatizo zaidi, nimuachie yeye timu,"amesema Matola.Matola amesema kwamba haoni mwelekeo wowote mzuri kwa Simba SC chini ya kocha huyu Muingereza ambaye hasikilizi ushauri, ndiyo maana ameamua kujitoa.

"Nimekutana na uongozi, nimewaambia juu ya uamuzi wangu, wakanisihi sana nisifanye hivyo, lakini nikashikilia msimamo wangu.

Wakaniambia hata nirudi kufanya kazi timu za vijana, lakini nikawaambia nitajifikiria kwanza" amesema Matola.

Matola aachia ngazi Simba SC.

Kocha msaidizi wa simba Suleiman Abdallah Matola amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na kile alichodai kutolelewana na Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan Kerr.

Matola amesema kwamba amefikia uamuzi huo baada ya kuona maelewano na bosi wake huyo yanazidi kuwa magumu kila kukicha."Ni jambo la muda mrefu, huyu kocha hasikilizi ushauri wangu, imefikia sasa ananichukia na kazi haziendi tena.

Sasa nimeona ili kuepusha matatizo zaidi, nimuachie yeye timu,"amesema Matola.Matola amesema kwamba haoni mwelekeo wowote mzuri kwa Simba SC chini ya kocha huyu Muingereza ambaye hasikilizi ushauri, ndiyo maana ameamua kujitoa.

"Nimekutana na uongozi, nimewaambia juu ya uamuzi wangu, wakanisihi sana nisifanye hivyo, lakini nikashikilia msimamo wangu.

Wakaniambia hata nirudi kufanya kazi timu za vijana, lakini nikawaambia nitajifikiria kwanza" amesema Matola.

MEMPHIS DEPAY NA MIPANGO YA KURUDI KWENYE KIWANGO

Depay: "Khali Ni Ngumu Unapokuwa Benchi,Lakini Ni Nzuri Kwa Sasa Na Itakuwa Nzuri Mazoezini Pia. Kwahiyo Nikipata Nafasi Ya Kucheza.,Nitaitumia"

Depay: "Mambo Mengi Yamebadilika.,Niko Kwenye Klabu Mpya Kwa Sasa, Na Ligi Ya Kiwango Tofauti Na Ya Uholanzi"

Depay: "Vitu Kama Hivyo Vinaathiri Unapokuwa Unajaribu Kuzoea.,Mwanzoni Ilikuwa Rahisi Kidogo Lakini Nikarudi Nyuma,Ilionekana Hata Kwa Jinsi Nilivyocheza"

Depay: "Hata Hivyo Niko Najituma Kwa Bidii Ili Niweze Rudi Kwenye Kiwango.
,Najisikia Vizuri Na Najaribu Kuonyesha Mazoezini Kwamba Nafanya Kadri Ya Uwezo Wangu Kucheza Vizuri"Mwanzoni Kijana Hakuitwa Timu Ya Taifa Ya Uholanzi Baada Ya Kocha Danny Blind Kudai Hachezi Kitimu.

Depay: "Nilipoongea Na Kocha Tulikuwa Na Maongezi Mazuri.,Nafikiri Nacheza Kitimu Na Nadhani Hata Wachezaji Wenzagu Wanafikiri Hivyo"

Depay: "Sidhani Kama Niko Katika Wakati Mgumu Wa Maisha Yangu Ya Soka Kama Wanahabari Wanavyosema.Lakini Nadhani Kiwango Changu Si Kizuri Sana Kwa Sasa"

Depay: "Naendelea Kujituma Kwa Bidii.,Tu Kwa Sababu Sijaonyesha Kiwango Changu Cha Kwenye Kombe La Dunia Ama Msimu Ulopita Haimaanishi Sijitumi Kwa Bidii"

Depay: "Sasa Najisikia Vizuri Na Watu Hawaoni Nnachokifanya Mazoezini,Watu Wanadhani Siko Bize Na Soka Lakini Hilo Si Kweli"