Facebook

Thursday 12 November 2015

MEMPHIS DEPAY NA MIPANGO YA KURUDI KWENYE KIWANGO

Depay: "Khali Ni Ngumu Unapokuwa Benchi,Lakini Ni Nzuri Kwa Sasa Na Itakuwa Nzuri Mazoezini Pia. Kwahiyo Nikipata Nafasi Ya Kucheza.,Nitaitumia"

Depay: "Mambo Mengi Yamebadilika.,Niko Kwenye Klabu Mpya Kwa Sasa, Na Ligi Ya Kiwango Tofauti Na Ya Uholanzi"

Depay: "Vitu Kama Hivyo Vinaathiri Unapokuwa Unajaribu Kuzoea.,Mwanzoni Ilikuwa Rahisi Kidogo Lakini Nikarudi Nyuma,Ilionekana Hata Kwa Jinsi Nilivyocheza"

Depay: "Hata Hivyo Niko Najituma Kwa Bidii Ili Niweze Rudi Kwenye Kiwango.
,Najisikia Vizuri Na Najaribu Kuonyesha Mazoezini Kwamba Nafanya Kadri Ya Uwezo Wangu Kucheza Vizuri"Mwanzoni Kijana Hakuitwa Timu Ya Taifa Ya Uholanzi Baada Ya Kocha Danny Blind Kudai Hachezi Kitimu.

Depay: "Nilipoongea Na Kocha Tulikuwa Na Maongezi Mazuri.,Nafikiri Nacheza Kitimu Na Nadhani Hata Wachezaji Wenzagu Wanafikiri Hivyo"

Depay: "Sidhani Kama Niko Katika Wakati Mgumu Wa Maisha Yangu Ya Soka Kama Wanahabari Wanavyosema.Lakini Nadhani Kiwango Changu Si Kizuri Sana Kwa Sasa"

Depay: "Naendelea Kujituma Kwa Bidii.,Tu Kwa Sababu Sijaonyesha Kiwango Changu Cha Kwenye Kombe La Dunia Ama Msimu Ulopita Haimaanishi Sijitumi Kwa Bidii"

Depay: "Sasa Najisikia Vizuri Na Watu Hawaoni Nnachokifanya Mazoezini,Watu Wanadhani Siko Bize Na Soka Lakini Hilo Si Kweli"

0 comments:

Post a Comment