Facebook

Thursday 12 November 2015

Suleiman Matola aachia ngazi Simba SC.

Kocha msaidizi wa simba Suleiman Abdallah Matola amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na kile alichodai kutolelewana na Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan Kerr.

Matola amesema kwamba amefikia uamuzi huo baada ya kuona maelewano na bosi wake huyo yanazidi kuwa magumu kila kukicha."Ni jambo la muda mrefu, huyu kocha hasikilizi ushauri wangu, imefikia sasa ananichukia na kazi haziendi tena.

Sasa nimeona ili kuepusha matatizo zaidi, nimuachie yeye timu,"amesema Matola.Matola amesema kwamba haoni mwelekeo wowote mzuri kwa Simba SC chini ya kocha huyu Muingereza ambaye hasikilizi ushauri, ndiyo maana ameamua kujitoa.

"Nimekutana na uongozi, nimewaambia juu ya uamuzi wangu, wakanisihi sana nisifanye hivyo, lakini nikashikilia msimamo wangu.

Wakaniambia hata nirudi kufanya kazi timu za vijana, lakini nikawaambia nitajifikiria kwanza" amesema Matola.

0 comments:

Post a Comment