Wednesday, 16 April 2014
Dau Kubwa Latangazwa Na Polisi Kwa Atakayeweza kutaja Waliohusika Katika Milipuko Ya Mabomu Arusha
Dau Kubwa la shilingi Milioni 10 limetangazwa na Jeshi la Polisi Tanzania kwa atakayewezesha kupatikana kwa wahalifu waliohusika katika milipuko ya mabomu Arusha wiki iliyopita.
Mkurugenzi wa makosa ya jinai Tanzania Dci Isaya Mgula amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na wataalam wa mabomu kutoka Jwtz na Jeshi la Polisi Tanzania umebaini bomu hilo limetengenezwa kienyeji.Bomu lililipuka kwenye Bar Ya Night Park na kusababisha madhara makubwa hasa majeraha kwa raia mbalimbali.
Bomu lingine lilikuwa limetegwa kwa kuegeshwa Pembeni ya kiti kwenye Bar Ya Washington iliyokuwa jirani
0 comments:
Post a Comment