KOCHA
mkuu wa Bayern Munich, Pep Gaurdiola anaamini klabu yake itakabiliana
na changamoto ngumu katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza, ligi ya mabingwa barani Ulaya hapo kesho dhidi ya Real Madrid.
Timu
hizo mbili zitaumana uso kwa uso katika fainali ya kwanza kwenye uwanja
wa Santiago Bernabeu na kocha huyo wa zamani wa Barcelona anaamini kuwa
hata kama Cristiano Ronaldo atakosekana, bado hakutaathiri ubora wa
wenyeji wao.
“Madrid
ni timu ya pekee kwa sasa ikiwa na Carlo Ancelotti. Ni klabu ngumu
zaidi tunayokutana nayo katika hatua hii”. Guardiola aliwaambia
waandishi wa habari.
“Mara
zote ninafurahi kucheza nusu fainali ya UEFA, hususani na timu kama
Madrid nikiwa na klabu kama Bayern. Tunahitaji kucheza vizuri na kupata
matokeo”.
“Tuna
matumaini ya kuonesha burudani kwa mashabiki. Watu wataona mambo mazuri
na kama Cristiano atacheza basi wategemee burudani zaidi”.
“Hata kama Ronaldo hayuko fiti, kuna wachezaji wengine wakali kama vile Isco. Bado itakuwa shughuli pevu”.
Kocha
huyo wa zamani wa Barcelona anashikilia rekodi ya kutofungwa katika
uwanja wa Bernabeu, lakini amegoma kutumia historia hiyo kueleka mchezo
wa kesho jumatano.
“Takwimu
hizo ni za zamani wakati nikiwa na klabu nyingine na sasa nipo na klabu
nyingine. Wala hazina uhusiano na mechi ya kesho”.
0 comments:
Post a Comment