"Habari inayoenezwa kuwa viongozi wakuu
wa UKAWA na hata waandamizi nikiwemo mimi, eti tumembembeleza mhe. Zitto
Kabwe ili aunge mkono mikutano ya UKAWA kuzunguka nchi siyo taarifa
zenye ukweli wowote.Mhe Zitto hajawahi kufuatwa na viongozi
kuombwa ashiriki ktk shughuli za UKAWA. Na hadi sasa UKAWA haijatangaza
shuguli zozote zile zaidi ya mkutano wa Zanzibar ambao pia polisi
wamekataa usifanyike leo hadi mara nyingine.Kwa bahati nzuri, wakati mhe. Zitto Z
Kabwe akichangia sura ya 1 na ya 6 bungeni, alionesha njia sahihi kwa
taifa na kwa asilimia mia moja aliunga mkono hoja za wananchi na hata
mapendekezo ya UKAWA.....Kwa mfano Zitto Kabwe alisema, "hoja ya
serikali tatu kuvunja muungano siyo ya kweli. Alisisitiza kuwa muungano
unaweza kuvunjika ndani ya serikali moja, mbili, tatu na hata tano"
Ujumbe wa UKAWA ni HIYARI. Ndiyo maana
baadhi ya wajumbe kama ISACK CHEYO wali-walk out pamoja na UKAWA bungeni
lakini keshoye walirejea na kuendelea na bunge.Umoja huu unaheshimu haki wajibu na maamuzi ya kila mtu. Msimamo wa UKAWA ni kulinda na kutetea rasimu ya maoni iliyoletwa na tume ya mabadiliko ya katiba kwa msingi wa kulinda mamlaka na maoni ya wananchi.
Tutafanya kazi na mtu yeyote ambaye anaamini yale tunayoyasimamia. Hatutamuomba mtu yeyote asiyeona uzito wa hoja zetu atuunge mkono, badala yake tutaendelea kuwaheshimu wote wanaotofautiana nasi kwa hoja huku tukiendelea kupigania kile ambacho tunakiamini."
J. Mtatiro,
UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI(UKAWA),
Zanzibar
0 comments:
Post a Comment