Thursday, 24 April 2014
Ivo.."Ntaliacha taulo linalowapa kiwewe wapinzani"..............fuatilia hapa................
INAWEZA kuwa habari njema kwa timu zitakazocheza na Simba msimu ujao wa Ligi Kuu Bara au mechi za kirafiki.
Kipa wa timu hiyo, Ivo Mapunda amesema ataacha kulitumia taulo lake katika michezo atakayocheza ili kuwatoa wasiwasi mashabiki wa timu pinzani.
Tangu alipokuwa akiichezea Gor Mahia ya Kenya msimu uliopita, Mapunda amekuwa akitumia taulo ambalo hulitundika katika nyavu za goli analodaka ili kujifuta jasho mikono yake pindi inapoonekana kuwa inateleza kuokoa mashuti ya timu pinzani.
Hata hivyo, mashabiki wengi wamekuwa wakilihusisha taulo hilo na imani za kishirikina.
Taulo la Mapunda liliibua tafrani Jumamosi iliyopita katika mchezo wa Simba na Yanga uliochezwa Uwanja wa Taifa, baada ya dakika 56 Yanga kukosa bao la wazi huku kipa huyo akiwa ametoka langoni ambapo kila walipopiga mpira ulikuwa ukiwagonga mabeki wa Simba.
Ndipo Didier Kavumbagu akalifuata taulo hilo na kwenda kulirusha kwa mashabiki wa timu yake japokuwa halikuweza kuwafikia.
Mapunda alisema: “Nimeamua kuachana na taulo langu ili kuwatoa wasiwasi wapinzani wangu, unajua wengi wanadhani lina mambo ya uchawi sasa ili wacheze wakiwa huru na kujituma sitaingia nalo uwanjani badala yake nitabuni kitu kingine ambacho kitakuwa maarufu kama taulo.
“Ninachofanya ni kuwapa burudani mashabiki wala hakuna kitu kingine cha ziada, lakini watu hawaelewi tazama Yanga walivyogombea taulo langu, mataulo yangu yote hayana uchawi wowote.”
Related Posts:
Man City yaua,yakaribia kileleni................ LEO Yaya Toure ameiongoza Manchester City vyema kwenye Mechi yao ya Ugenini dhidi Crystal Palace na kuisaidia kushinda kwa magoli 2-0 na kuwakaribia Vinara Liverpool sasa wakiwa Pointi 3 nyuma yao na Mechi moja mkononi. … Read More
Tanzania yaichapa Kenya 4-3................ Timu ya taifa ya soka ya Tanzania kwa vijana wenye umri wa miaka 20 imesonga mbele kwenye safari ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la mataifa baada ya kuilaza Kenya kwa mikwaju ya Pena… Read More
Atletico Madrid yashinda,yaukaribia ubingwa.............. WAKICHEZA Ugenini huko Estadio de Mestalla, Vinara wa La Liga, Atletico Madrid wameifunga Valencia goli 1-0 na kupaa kileleni wakiwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili, Real Madrid. Atletico,ambaoJumatano wanasafiri… Read More
Yondani atemwa Taifa Stars,Kapombe, Bocco na Cannavaro waitwa............. Kocha mpya wa Taifa Stars, Mart Nooij ameongeza wachezaji tisa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi (The Fla… Read More
Carlo Anceloti:Madrid iko tayari kuivaa Bayern 100%.................. CARLO Ancelotti anaamini kuwa hali ya hewa iliyopo Real Madrid kwa sasa inatosha kuwapa ushindi dhidi ya Bayern Munich kesho kutwa (jumanne) kwenye nusu fainali ya pili y… Read More
0 comments:
Post a Comment