Monday, 21 April 2014
Je !!! Wajua..Kumbe Rais hana mamlaka ya kuwafukuza "UKAWA" bunge la katiba na kuchagua wengine........fuatilia hapa...........
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema Rais Jakaya Kikwete hana uwezo kisheria wa kuwafukuza au kutengua uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
Jaji Werema alisema Sheria namba 8 ya Mabadiliko ya Katiba ya 2011, ipo kimya kuhusu suala hilo na kwamba kwa maana hiyo Rais hana mamlaka ya kutengua hata ubunge wa wale aliowateua kupitia kundi la wajumbe 201.
“Umesoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba? Kaisome maana ili mtu afukuzwe ubunge lazima apungukiwe sifa za nafasi hiyo, lakini kama sheria iko kimya maana yake ni kwamba hana (Rais) uwezo wa kuwafukuza,” alisema Jaji Werema.
Jaji Werema alikuwa akijibu maswali ya gazeti hili kuhusu hatima ya wajumbe ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao Jumatano jioni waliondoka bungeni kwa madai ya kutoridhishwa na uendeshaji wa Bunge Maalumu.
Wajumbe waliotoka nje ni wanaotokana na vyama vya CUF, Chadema, NCCR Mageuzi, NRA, NLD na baadhi kutoka kundi la 201. Alhamisi asubuhi, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta alisema utafiti uliofanywa na ofisi yake ulibaini kuwa katika kundi la 201, ni wajumbe 25 tu ambao walitoka nje pamoja na Ukawa.
Baada ya wajumbe hao kutoka nje, Mjumbe wa Bunge hilo, Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, aliomba mwongozo akihoji iwapo Ofisi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu haiwezi kumwandikia Rais Kikwete ili ateungue uteuzi wa wajumbe katika kundi la 201 ambao waliungana na Ukawa kususia vikao.
“Ningependa Rais atengue hadhi zao ili kuingiza watu wengine ambao wako tayari kufanya kazi hata bure, sisi tunalipwa fedha nyingi, lakini tunaleta mzaha, watu hawana maji, dawa, madawati, ada za elimu ya juu watu wamekosa, hizi fedha zingetumika huko,” alisema Nchemba mwenye wadhifa mwingine wa Naibu Waziri wa Fedha.
Matakwa ya Sheria
Jaji Werema alisema: “Ili mtu aondolewe katika nafasi yake ni lazima akose sifa za kuwa mjumbe, mathalan kuugua ugonjwa wa akili au kichaa, kuumwa muda mrefu kiasi cha kushindwa kutimiza majukumu yake na kadhalika, lakini sifa hizo kama hazipo kwenye sheria sasa unaanzia wapi?”
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2011 pamoja na marekebisho yake ya 2012 na 2013 inawataja Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kwa mujibu wa nafasi zao.
Kadhalika sheria hiyo inampa Rais mamlaka ya kufanya uteuzi wa wajumbe 201 kutoka makundi mbalimbali, lakini haitaji sifa wanazopaswa kuwa nazo wajumbe hao.
Jaji Werema alisema hata kama sheria ingekuwa inaruhusu kufukuzwa au kusitishwa kwa ujumbe wa wabunge hao, hakuna sababu ya msingi ya kuwachukulia hatua hiyo.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali kuhusu sakata la katiba mpya kwa wakati sahihi
Related Posts:
Use any SIM CARD in any MODEM without unlocking it Ni shida sana watu wanakuwa nayo kila mtu anataka Ku-unlock Modem yake ili aweze kuitumia laini tofauti na mtandao mmoja husika wa hiyo modem,. Sasa leo wanacomplex tunawekana sawa hapa jinsi ya kutumi… Read More
100's SAMSUNG SECRET CODES Kwa wale wanaotumia simu za Android basi hizi hapa ni codes ambazo unaweza kuweka na kuona maajabu! * Software version: *#9999# * IMEI number: *#06# * Serial number: *#0001# * Battery status- Memory capacity : … Read More
IP ADDRESS FULL KNOWLEDGE An IP address is an identifier for a computer or device on a TCP/IP network. Networks using the TCP/IP protocol route messages based on the IP address of the destination. The Format of an IP Address T… Read More
Jifunze hapa "NETWORK SKILLS" Introduction A network is a collection of computers and devices connected to each other. The network allows computers to communicate with each other and share resources and information. History of Netw… Read More
Zitambue simu fake na Original SAMSUNG GALAXY S3 Mambo vipi wadau, naamini tuko salama sote. Leo ningependa kushare nanyi kitu ambacho kimezoeleka sana kuwanacho kwenye mikono yetu lakini kuna kipindi ukikihitaji kile kilicho bora lazima utaikumbuka hii POST.… Read More
0 comments:
Post a Comment