Facebook

Thursday, 24 April 2014

Mourinho,msaidizi wake na Ramires hatarin kupewa adhabu kali na FA...................fuatilia hapa..........


MOURINHO-FARIA_VURUGU 
MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho, na Msaidizi wake, Rui Faria, pamoja na Mchezaji wao Ramires, wamefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kufuatia matukio kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Wikiendi iliyopita Chelsea walipopigwa Bao 2-1 na Sunderland Uwanjani Stamford Bridge.
Wakati Mourinho anatuhumiwa kutoa kauli ambayo inahoji uadilifu wa Refa wa Mechi hiyo, Mike Dean, Rui Faria ameshitakiwa kwa Utovu wa Nidhamu kufuatia kuzuka zogo baada ya Sunderland kupewa Penati na kumfanya Refa Mike Dean amtoe nje Msaidizi huyo wa Mourinho lakini akagoma na kulazimisha kuvutwa ili atoke.
Ramires yeye ameshitakiwa kwa kucheza kwa fujo baada ya kunaswa akimpiga Mchezaji wa Sunderland Sebastian Larsson wakati Mpira haupo kwao na bila Refa Mike Dean kuona tukio hilo.
Kwa sababu Ramires tayari ameshatolewa nje kwa Kadi Nyekundu mara mbili Msimu huu, huenda safari hii akakumbwa na Kifungo cha Mechi 5.
Mourinho na Faria wamepewa hadi Jumatatu Aprili 28 kujibu Mashitaka yao na Ramires anatakiwa ajibu ifikapo Alhamisi Aprili 24.

0 comments:

Post a Comment