Facebook

Tuesday, 22 April 2014

Moyes kufuzwa kazi muda wowote kuanzia sasa.........fuatilia hapa.....

388907_heroa


Vyombo vya habari vya Uingereza, likiwemo Mail on Sunday vimeripoti kuwa David Moyes ataachishwa kazi wiki chache zijazo na kwamba anaweza kuachiswa hata leo au kesho

Wamiliki wa timu hiyo, familia ya Glazer wanadaiwa kuishiwa uvumilivu kwa kocha huyo ambaye tangu aanze kuinoa imeendelea kufanya vibaya na sasa ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa Barclays Premier League. Jana Man United ilifungwa mabao 2-0 na Everton.


Uongozi wa juu wa klabu ulikuwa umepania kumpa muda kocha huyo lakini umeona ni ngumu kuona mabadiliko kwakuwa hata wachezaji hawamwamini tena kocha wao. Ripoti hizo zinadai kuwa nafasi yake inaweza ikachukuliwa kwa muda na Ryan Giggs huku makocha wanaowaniwa kuchukua nafasi ya muda wote wakitajwa kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp, kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal na kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kujua hatma ya David Moyes ndani ya Manchester United fc ......... 

0 comments:

Post a Comment