Msamaha wamnusuru kunyongwa Iran
Mamake mmoja muathiriwa alimzaba kofi mtuhumiwa na kisha kumasamehe dakika chache kabla ya kunyongwa
Mtu mmoja aliyehukumiwa kifo kwa
kunyongwa nchini Iran baada ya kupatikana na hatia ya mauaji, ameponea
chupuchupu baada ya kusamehewa na mamake muathiriwa.
Mama huyo alimsamehe mtuhumiwa dakika chache tu kabla ya kuwekwa kamba shingoni.
Picha za tukio hilo zilipigwa moja kwa moja na
mpiga picha mmoja aliyenasa kila hatua ya tukio hilo ambalo
liliwashangaza wengi nchini Iran na duniani kote.
Balal alimuua kwa kumdunga kisu Abdollah Hosseinzadeh miaka saba iliyopita
Shirika la habari la ISNA nchini Iran liliripoti
kuwa mtuhumiwa huyo, kwa jina Bilal, alihukumiwa kifo baada ya kumuua
kijana mmoja Abdollah Hosseinzadeh, wakati wawili hao walipokuwa
wanapigana katika soko moja mjini Nour miaka saba iliyopita.
Bilal alifikishwa katika sehemu ya kunyongewa akiwa amefunikwa macho yake tayari kwa hukumu kutekelezwa siku ya Jumanne.
Lakini dakika ya mwisho kabla ya kunyongwa,
mamake mwathiriwa Samereh Alinejad, alimwambia kuwa amemsamehe baada ya
kuhutubia umati uliofika kushuhudia hukumu hiyo , kisha akamzaba kofi
Bilal kabla ya Bilal kunusurika kifo.
Samereh Alinejad, mamake marehemu Abdollah Hosseinzadeh, alimzaba kofi Balal dakika za mwisho alipokuwa anasubiri hukumu
Kisha alimuondoa kamba shingoni akisaidiwa na mumewe.
Kabla ya mama huyu kumsamehe Balal alihisi hisia kali baada ya kukumbuka kifo cha mwanawe
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kufahamu matukio mbalimbali yanayotokea duniani kwa wakati muafaka
0 comments:
Post a Comment