Facebook

Saturday, 19 April 2014

Baada ya Meli kuzama,leo hii wapigambizi wameenda kuwasaka manusura.......soma hapa......



Wapiga mbizi wa Korea kusini wamefanya majaribio kadhaa yakuingia ndani ya feri ya abiria iliozama siku ya jumatano,lakini mawimbi makali na kutoona vizuri kunaathiri shughuli yao ya kuisaka miili ya waathiriwa.
Afisa mmoja wa walinzi wa pwani ya taifa hilo amesema kuwa kundi moja la maafisa wake lilifanikiwa kuona miili mitatu ya watu katika dirisha moja la feri hiyo ,lakini wakashindwa kuvunja kioo cha dirisha hilo kuchukua miili hiyo.
Wapiga mbizi hao wakitumia kamba za kuwaelekeza wamelifikia eneo la juu la chombo hicho ,lakini wameshindwa kuingia katika vyumba vyake.
Zaidi ya watu 270 wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule hawajulikani waliko.
Nahodha wa ferry hiyo na wafanyikazi wenzake wamekamatwa.

0 comments:

Post a Comment