MCHEKESHAJI maarufu hapa nchini katika
swaga za kimasai ambaye pia ni mmiliki wa masainyotambofu.info Gilliady
Severine Kahema 'Masai Nyotambofu' Ameamua kuitema kampuni aliyokuwa na
mkataba nayo ya Al-Riyamy Pro ambayo hurusha kipindi chake cha VITUKO
SHOW kwenye runinga ya CHANNEL TEN.
Akizungumza leo, Masai Nyotambofu alisema kuwa ameamua kuachana na kampuni hio baada kugundua kuwa kuendelea kuwepo pale kwa muda mrefu ni sawasawa na kuididimiza sanaa yake kwani hamna mafanikio yeyote zaidi ya kuahidiwa kwamba baada ya kipindi fulani mambo yatakuwa mazuri huku siku zinazidi kwenda, ''Kiukweli nimeamua kuachana na Al-Riyamy Pro maana naona muda wote wa miaka mitano sijafikia malengo yangu niliotarajia na ahadi za kampuni hazionekani,
Pia kikubwa zaidi kilichoniondoa ni pamoja na kuchezeshwa na wasanii wasio na vipaji halisi wanaishia kuigaiga stile za watu tu hatima yake tunaonekana wote wabovu. Hapo mwanzo tulivyokuwa timu kamili tulifanya vizuri na kupokelewa vizuri lakini walivyoondoka baadhi ya wasanii wenye uwezo mkurugenzi akasema analeta wasanii wengine, Basi mimi nikaendelea kusubiri maana kila msanii alikuwa na mkataba wake hivyo kila aliyeondoka aliondoka kwa sababu zake binafsi mimi nikaendelea kukomaa nikihisi mbele ya safari kutakuwa na mabadiliko, Mara mkurugenzi akaaza kuwaleta watu tu from no whwre wasio na vipaji vya sanaa tucheze nao, Kila nikimuuliza kuwa mbona wengine wakisimama mbele ya Camera wakiambiwa Action hawajui itakuwaje? Jibu lake alinijibu nawasaidia maisha yao magumu. Nikamwambia huoni kuwa kazi ikiwa mbovu tutapoteza mashabiki? Akajibu we fanya kazi ntapitisha mchujo wasio na vipaji ntawaondoa watabaki wenye vipaji wachache tu niwatengenezee maisha ili muuone umuhimu wa kukaa kwenu hapa miaka mingi mimi nauona uvumilivu wenu, Cha ajabu mkurugenzi aliendea kujaza watu wasio na vipaji uongozi hakuna nidhamu kambini mbovu mimi siheshimiwi na mimi simuheshimu mtu basi tafrani kama kilabu cha komoni. Lakini nikaendelea kukomaa nikitarajia mabadiliko mwaka 2014, Kuna siku nikajaribu kumwambia mkurugenzi kuwa aniazime kiasi fulani cha fedha nikamilishe Video ya wimbo wangu alafu anikate akasema sina hela huoni mko wengi? kwanza kampuni hainilipi wewe unataka upate promo ili uzidi kuitwa kwenye Show utashuti saa ngapi na kwenye Show utaenda saa ngapi? Dah! Hapo ndipo nilipoona kuwa napoteza muda ukizingatia mwanzoni tulivyokuwa wakali watupu kipindi kikiruka hewani simu za wasanii zinaita mpaka kero lakini sasahivi kipindi kinaruka mwanzo mwisho hata hubipiwi..! Ni ishara tosha kwamba watazamaji wameanza kuingia mitini. Ni bora nikae pembeni nikinusuru kipaji changu kwani kama riziki yangu mwenyezi mungu hakuniandikia kuipata hapo hata nikomae vipi kamwe sitofanikiwa hapo. Nimeamua kurudi Nyumbani Jijini Dar kutuliza kichwa sina mkataba na kampuni yeyote kwa sasa najiandaa kuachia ngoma mpya baada ile niliyomshirikisha Rich Mavoko na Kitokololo (Yero Masai) Watu wangu kaeni mkao wa kula Uchekeshaji siachi mpaka mwisho wa uhai wangu, Kuondoka Al-Riyamy Pro Sio mwisho wa kampuni kufanya kazi wataendea wengine na wala sio mwisho wangu wa kuchekesha bado mtaendela kuzipata ladha zangu kupitia filamu zangu ambazo nipo katika mikakati ya kuanzisha Project. Namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa kipaji hiki kilichonifanya niwe na ukaribu wa hali ya juu na watu mbali mbali na katika show zangu napokelewa vizuri hicho kinanifanya nimuheshimu kila mtu wa kila rika, Nawapenda Mashabiki wangu One Love.

0 comments:
Post a Comment