Mshambuliaji wao raia wa Brazil, Neymar ataa nje ya uwanja wa
wiki nne, wakati naye beki Jordi Alba atakaa muda kama huo baada ya wote
kupata majeruhi.
Klabu
ya Barcelona imethibitisha kuwa Neymar alipata majeruhi ya mguu jana
katika mchezo wa fainali ya kombe la Mfalme dhidi ya Real Madrid.
Kinda
huyo mwenye miaka 21 alishindwa kuisaidia Barca kuepukana na kipigo cha
mabao 2-1, huku Mbrazil huyo akikosa nafasi ya wazi dakika za lala
salama.
Neymar atakosa mechi zijazo dhidi ya Athletic Bilbao, Villarreal, Getafe na Elche.
Hata hivyo klabu ya Barca ina matumaini kuwa nyota wake huyo anaweza kurudi katika mechi ya mwisho dhidi ya Atletico Madrid.
Taarifa
ya klabu ya Barcelona imesema;”Mchezaji huyu aliumia jana katika mguu
wake wa kushoto na anahitaji muda maalumu wa matibabu. Makadirio ya
kurudi uwanjani ni wiki nne”.
Naye
Jordi Alba alitolewa baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza katika
mechi ya jana na taarifa zinaeleza kuwa beki huyo wa kushoto aliumia
nyama za paja za mguu wake wa kulia.
Beki huyo wa zamani wa Valencia anaweza kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu hadi nne
0 comments:
Post a Comment