Facebook

Saturday, 19 April 2014

Brenden Rodgers adai Gerrard ndiye kiungo bora kabisa Ulaya kwa sasa....fuatilia hapa.....

379947_heroa
KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers anaamini kuwa nahodha wake, Steven Gerrard ndiye kiungo na kiongozi bora zaidi barani Ulaya.
Rodgers amesema japokuwa Gerrard mwenye umri wa miaka 33 hajacheza mechi zote za ligi kutokana na majeruhi, lakini amefanya kazi kubwa kuisukuma timu kwenda mbele katika harakati za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
‘Kuna wakati kiwango cha Gerrard kinapotea kutokana na kutumia muda mwingi kuwaongoza wenzake katika timu. Uongozi wake umetukuka kweli”
“Hakuna wachezaji wengi wanaoweza kufanya kazi kama Gerrard. Ni mzuri kwa kushambulia na kuzuia eneo la kati”.
“Naangalia wachezaji wengi wanaocheza nafasi kama ya Gerrard katika klabu za juu, lakini sijaona kama yeye, kwasababu anaipa timu kile inachohitaji”.

0 comments:

Post a Comment