Facebook

Saturday, 19 April 2014

Moyes aomba heshima kwa mashabiki wa Everton kesho...soma hapa....

392540_heroa

KOCHA wa zamani wa Everton na sasa Manchester United, David Moyes anaamini kuwa anastahili heshima kutoka kwa mashabiki  wa klabu yake hiyo ya zamani katika mchezo wa ligi kuu hapo kesho uwanja wa Goodison Park.
Mscotishi huyo alizomewa na mashabiki waliosafiri kwenda Old Trafford  katika mchezo wa mzunguko wa kwanza mwezi desemba mwaka jana, lakini bado anajivunia mafanikio aliyoyapa alipokuwa Goodison Park.
Moyes aliyeondoka katika klabu hiyo Merseyside mwishoni mwa msimu wa mwaka jana alizomewa na mashabiki ambao waliona kama amepotea njia.
“Walikuw ana sababu yao ya kunizomea mwezi desemba”.
“Kulitokea matatizo machache  pale nilipojaribu kuwasajili wachezaji wao, lakini yote kwa yote nilikuwa nafanya kazi yangu Manchester United”.
“Tulitumia fedha nyingi kusajili wachezaji nilipokuwa Everton na kuboresha timu, Nadhani tulijitahidi kwa nguvu zote kuijenga timu hii”.
“Mchezo haunihusu mimi. Ni mechi ya timu mbili zinazohitaji ushindi”.
“Malengo yao yasiwe juu yangu mimi, waangalie wachezaji wao, lakini najua mashabiki wa Everton wana haki ya kufanya watakavyo”. Alisema Moyes.
Moyes alitumia pauni milioni 27.5 kumsajili kiungo Marouane Fellaini kutoka Everton katika siku ya mwisho ya usajili.
Pia alikuwa anamtaka beki wa kushoto wa klabu hiyoLeighton Baines.

0 comments:

Post a Comment