WINGA
machachari wa Chelsea, Eden Hazard yuko hatarini kukosa mechi ya kwanza
ya nusu fainali ya UEFA dhidi ya Atletico Madrid kutokana na
kusumbuliwa na majeruhi.
Hazard
alitolewa katika mchezo wa robo fainali dhidi ya PSG ambapo walishinda
mabao 2-0 na kufuzu nusu fainali kwa wastani wa mabao 3-3, lakini
Chelsea walikuwa na faida ya bao la ugenini.
Kocha
msaidizi wa Chelsea Steve Holland mapema wiki hii alisema Hazard
anaendelea vizuri na anaweza kucheza, lakini taarifa za leo ijumaa ni
mbaya zaidi kwasababu nyota huyo hatakuwa fiti kwa mechi hiyo.
“Sio
kwamba Hazard hataweza kuimarika, lakini kushindwa kufanya mazoezi na
timu inaashiria wasiwasi kwa yeye kucheza”. Alisema taarifa ya Holland
kwa waandishi wa habari.
Kabla
ya kwenda kucheza nusu fainali ya UEFA katika uwanja wa Vicente
Calderon, Chelsea watasafiri kuwafuata vibonde wa ligi kuu soka nchini
England, klabu ya Sunderland, mechi inayoaminika kuweka wazi kama
Mourinho ataendelea kuwepo katika mbio za ubingwa.
Katikati
ya wiki, mashabiki wa soka walishuhudia Sunderland wakiwakazia
Manchester City na kutoka sare ya 2-2, lakini kama Chelsea watashinda
mechi hiyo na nyingine zote zilizobaki wanaweza kuwa katika nafasi nzuri
ya kubeba mwari.
Holland
aliendelea kwa kusema: “nafasi ya kwanza, pili na tatu inawezekana kwa
timu zote tatu za juu. Timu zinakaribiana sana kwa pointi. Lakini ndio
timu iliyocheza mechi nyingi zaidi msimu huu”.
“Ni
msimu wenye changamoto kubwa, hakika unaumiza kichwa sana. Nadhani
uzoefu ni muhimu katika mashindano yoyote yale. Tunao wacheza wenye
uzoefu kwenye kikosi, nadhani watatusaidia”.
“Mechi
ya kesho ni muhimu mno kwetu. Siamini kama ubingwa wa msimu huu
utaamuriwa katika mechi yetu na Liverpool. Mchezo wa kesho na Sunderland
ni mgumu zaidi na tunahitaji kuingia kwa umakini mkubwa”
Endelea kutembelea www.katemimethsela.blogspot.com kwa habari za undani zaidi zilizo kamili
0 comments:
Post a Comment