Chelsea 1-2 Sunderland Fc.
Rekodi nzuri ya Jose Mourinho ya kutofungwa katika Mechi 78 za Ligi Kuu England Uwanjani Stamford Bridge Leo imevunjwa baada ya kuchapwa Bao 2-1 na Timu ya mkiani Sunderland na kuyaacha matumaini yao kutwaa Ubingwa mashakani huku Vinara Liverpool wakichekelea.
Sunderland bado wako mkiani lakini
Jumapili, Liverpool wakishinda watakuwa Pointi 5 mbele juu kileleni na
kubakiwa na Mechi 3 mojawapo ikiwa Wikiendi ijayo Uwanjani Anfield na
Chelsea na hapo wanaweza kabisa kutwaa Ubingwa kutegemea na Mechi
nyingine kabla ya hiyo.
Leo hii, Chelsea walitangulia kufunga kwa goli la Samuel Eto’o na Sunderland kusawazisha kwa goli hilo kupitia kwa Connor Wickham.
Goli la ushindi kwa Sunderland lilifungwa
kwa Penati ambayo Msaidizi wa Refa ndie alimuashiria Refa Mike Dean ni
Penati baada ya beki wa kushoto wa Chelsea Azpilicueta kuteleza na Mpira kunaswa
na Altidore ambae aliingia ndani ya Boksi na Azpilicueta kujaribu
kuuzuia Mpira lakini Altidore akajiangusha na Penati kutolewa.
Penati hiyo ilifungwa na Borini.
Tottenham 3 Fulham 1
-White Hart Lane
Bao za Paulinho, Kane na Kaboul
zimewapa Tottenham ushindi wa Bao 3-1 walipocheza na Fulham ambao kipigo
hiki kimezidisha wasiwasi wao wa kushushwa Daraja.
Bao pekee la Fulham lilifungwa na Steve Sidwell ambae pia alikosa Penati iliyookolewa na Kipa Hugo Lloris.
Cardiff City 1 Stoke City 1
-Cardiff City Stadium
Golio za Penati zimeifanya Mechi hii imalizike kwa Sare ya goli 1-1
Marko Arnautovic aliifungia Stoke kwa
Penati iliyotolewa kwa Faulo ya Kim Bo-Kyung kwa Peter Odemwingie na
Peter Whittingham kusawazisha kwa Penati kwa faulo iliyofanywa na Steven Nzonzi
kwa Fraizer Campbell.
Newcastle United 1 Swansea City 2
-Saint James’ Park
Penati ya Dakika za Majeruhi ya
Wilfried Bony imeipa ushindi wa magoli 2-1 Swansea City walipocheza
Ugenini na Newcastle na kuwapa matumaini makubwa ya kunusurika kushushwa
Daraja.
Newcastle ndio walitangulia kwa goli la Shola Ameobi lakini Wilfried Bony alisawazisha.
Wakati Mechi ikielekea kuwa Sare, katika
Dakika za Majeruhi Marvin Emnes aliangushwa na Cheick Tiote ndani ya
Boksi na Bony kufunga goli lake la Pili na la ushindi.
Refa Chris Foy ilibidi atolewe katika
Dakika ya Kwanza baada ya Shuti la Jonjo Shelvey kumbabatiza Usoni na
nafasi yake kuchukuliwa na Refa wa Akiba, Anthony Taylor.
West Ham United 0 Crystal Palace 1
-Upton Park
Crystal Palace wamejihakikishia kubaki
Ligi Kuu Engkand baada ya kuichapa West Ham United, waliokuwa kwao
Upton Park, goli 1-0 kwa Penati ya Mile Jedinak ya Dakika ya 59
iliyotolewa kufuatia Pablo Armero kumwangusha Cameron Jerome.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari za uhakika kwa muda muafaka......
0 comments:
Post a Comment