
JUMAMOSI
Old Trafford itashuhudia Historia mpya wakati Wachezaji wao Nguli, Ryan
Giggs, Nicky Butt, Phil Neville na Paul Scholes, watakapoiongoza Timu
wakiwa Benchi la Ufundi kwenye Mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya
Norwich City.
Mechi hii, ambayo sasa imeleta mvuto
mkubwa, pia itashuhudiwa na Famila ya Glazer, Wamiliki wa Man United,
ambao Leo hii wametua Manchester kufuatilia mchakato wa Meneja mpya.
Mara baada ya David Moyes kufukuzwa kazi
Juzi Jumanne na Ryan Giggs kuteuliwa kama Meneja wa Muda, Giggs
aliwaita wenzake Nicky Butt, Phil Neville na Paul Scholes kukaa nae
Benchi kumsaidia kuiongoza Man United kwenye Mechi zao 4 za Ligi
zilizobaki.
Wachezaji hao, pamoja na David Beckham
na Gary Neville, ndio waliounda Kikosi maalum cha Man United cha
Wachezaji Chipukizi kilicholeta mafanikio makubwa na kubatizwa ‘CLASS OF
92’ ikiashiria Mwaka walioibukia kuichezea Timu ya Kwanza ya Man
United.
Habari za ndani ya Old Trafford zinasema
kuwa mara baada ya Ryan Giggs kuteuliwa Meneja, aliwaambia Wachezaji
wakati umefika wa kurudi kucheza kama Manchester United, kushambulia
bila kuogopa Timu na kuzibana Timu bila kujali wao ni nani.
Nae Nicky Butt, ambae ndie alikuwa Kocha
wa Timu ya Rizevu ya Man United, ameiambia MUTV, Kituo cha TV cha Man
United, kuhusu Mechi yao na Norwich City kwamba: “Hii ni Gemu kubwa
kwetu na fahari kubwa kwetu. Kuwa pamoja ni kitu kisichoaminika.
Tuliingia hapa pamoja tukiwa na Miaka 12 na kwa sisi kuwa pamoja sasa ni
fahari kubwa mno!”
Butt alisisitiza kuwa Man United inao Wachezaji wazuri mno ambao wanaijali Timu yao na wanaitakia mema Klabu yao.
0 comments:
Post a Comment