Facebook

Wednesday, 23 April 2014

Homa yapanda Real Madrid vs Bayern Munich.......................fuatilia hapa.........

UCL-REAL_v_BAYERN 
Bayern Munich, Mabingwa Watetezi, wapo kwenye hatua muhimu ya utetezi wao wa Taji lao na wapo Ugenini Santiago Bernabeu huko Madrid dhidi ya Vigogo wa Spain, Real Madrid, wakihaha kuwa Klabu ya kwanza kutetea Taji la Ulaya tangu AC Milan wafanye hivyo Miaka ya 1990.

Wakati Bayern, chini ya Meneja wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, walitwaa Ubingwa wa Germany Mwezi uliopita, Real, chini ya Meneja Carlo Ancelotti, bado wanashindana na Atletico Madrid na Barcelona kutwaa Ubingwa wa Spain.

Mara ya mwisho kwa Timu hizi kukutana kwenye UCL ni kwenye Nusu Fainali ya Msimu wa 2011/12 ambapo Bayern walitinga Fainali kwa Mikwaju ya Penati baada kufungana Bao 2-1 Mechi ya Kwanza, kwa Bao za Franck Ribery na Mario Gomez kuipa ushindi Bayern, na Bao 2-1 huko Bernabeu kwa Bao mbili za Ronaldo kuipa ushindi Real.
Kwenye Mikwaju ya Penati, Bayern walishinda Penati 3-1 huku Kipa wa Bayern, Neuer, akiwa Shujaa kwa kuokoa Penati za Ronaldo na Kaka.
Real na Bayern zimekutana kwenye Nusu Fainali za UCL mara 5 na Bayern kushinda mara 4, Miaka ya 1976, 1987, 2001 na 2012, na Real kushinda mara 1 pekee Mwaka 2000.
Wakati Real wametwaa Kombe hili mara 9, na sasa wanasaka kulibeba mara ya 10, wenyewe wakiita ‘DECIMA’, Bayern wametwaa mara 5.
Pia, Real wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hawajapoteza Mechi 17 za Ulaya Uwanjani kwao Santiago Bernabeu na mara ya mwisho kufungwa hapo ni Msimu wa 2010/11 walipochapwa 2-1 na Barcelona kwenye Nusu Fainali.

Hali za Wachezaji:
Wachezaji wa Real Madrid ambao ni Majeruhi ni Álvaro Arbeloa , Sami Khedira na Jese.
Kwa Bayern Munich Majeruhi wao ni pamoja na Kipa wao Manuel Neuer, ingawa anaweza kucheza, Xherdan Shaqiri, Thiago Alcántara na David Alaba ambae anasumbuliwa na Mafua.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
REAL MADRID: Iker Casillas, Carvajal, Coentrao, Varane, Ramos, Alonso, Illarramendi, Modric, Di Maria, Ronaldo, Benzema

BAYERN MUNICH: Neuer, Lahm, Rafinha, Boateng, Dante, Kroos, Schweinsteiger, Robben, Gotze, Ribery, Mandzukic
 
REFA: Howard Webb  (England)

0 comments:

Post a Comment