Historia Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inaanzia April 26 mwaka 1964 siku ambayo Nchi ya Jamuhuri ya
Tanganyika ambayo kwa sasa ni Tanzania bara pamoja na iliyokuwa Jamuhuri
ya Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja) ziliungana na
kuwa nchi moja.
Kumbu kumbu zinaonyesha Jamhuri ya Tanganyika na
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliingia mkataba tarehe 22 Aprili 1964
huko Zanzibar kwa lengo la kuunganisha nchi hizo mbili baada ya kutiwa
saini na viongozi wa nchi hizo kwa wakati huo ambao ni aliyekuwa Rais wa
Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa
Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.Hata hivyo nchi hii mpya iliendelea kujulikana kwa jina hilo la"Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar" hadi Oktoba 28, 1964 lilibadilishwa rasmi kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jina linatumika hadi hivi leo kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.
Kwa ujumla Muungano huo wa kuunganisha nchi mbili kwa hiari umekuwa ukisifiwa kwamba ni Muungano wa kipekee barani Afrika Professa Paramagamba Kabudi Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yeye anasema katika utafiti wake amegundua ni Muungano huo ndio pekee wa hiari uliodumu hadi hivi leo.
Muundo wa Muungano uliokubaliwa
Nchi mpya iliyozaliwa yaani Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni muungano wenye Muundo wa vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji ambavyo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ambavyo ni Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma ambavyo ni Bunge la Jamuhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi.
Katika utekelezaji wa shughuli zake Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenyewe imepewa mamlaka ya kushughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Tanzania na mambo yale yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara huku Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenyewe imepewa mamlaka ya kushughulikia mambo yote yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Zanzibar.
Mambo ya Muungano
Mambo ya Muungano ya kwanza kabisa yaliyoanishwa kwenye Katiba ya muda ya mwaka 1965 yalikuwa ni 11 ambayo ni• Katiba na Serikali ya Muungano
• Mambo ya Nchi za Nje
• Ulinzi
• Polisi
• Mamlaka juu ya mambo yanohusika na hali ya hatari
• Uraia
• Uhamiaji
• Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje
• Utumishi katka Serikali ya Jamhuri ya Muungano
• Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
• Bandari mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.
Hata hivyo Baadae Mambo ya Muungano yaliongezeka kutoka kumi na moja (11) hadi ishirini na mbili (22)
Likiwemo suala la sarafu na benki kuu ambapo nchi zote zilianza kutumia sarafu moja hadi hivi leo.
Mbali na mafanikio yaliyopatikana Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa ukipitia safari ya mabonde na milima ambapo wapo wanao ona kuwa umewapa manufaa huku wengine wakidhani muungano hauna faida.
Kwa sasa Tanzania ipo kwenye mchakato wa kuandika Katiba Mpya ambapo suala la Muundo upi wa Muungano unaofaa kati ya Muundo uliopendekezwa kwenye rasimu ya Katiba wa serikali tatu na muundo wa sasa unaopigiwa debe na chama tawala wa serikali mbili ni mjadala uliopamba moto katika nchi hii.
Hata hivyo kwa vyovyote vile pamoja na changamoto na matatizo yote hayo ni wazi muungano huo kufikisha miaka 50 sio jambo dogo
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kujua hatma juu ya Muungano wa Tanzania......................
0 comments:
Post a Comment