Facebook

Tuesday, 22 April 2014

Messi kuongezwa mkataba Barca ................fuatilia hapa...................


MESSI-HETITRIKI-16MACHI
























MARA baada ya Jana Lionel Messi kuisaidia Barcelona kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kufunga Bao la Pili na la ushindi walipoifunga Athletic Bilbao Bao 2-1 kwenye Mechi ya La Liga na kuifanya Barca ikamate Nafasi ya Pili Pointi 4 nyuma ya Atletico Madrid, Rais wa Klabu hiyo, Josep Bartomeu, amesisitiza Staa huyo atapewa Mkataba mpya ili kumbakiza Klabuni hapo.

Kumekuwa na minong’ono kuwa Mchezaji huyo atahama Nou Camp baada ya Msimu huu kuwa mgumu kwake na kukabiliwa na maumivu ya mara kwa mara lakini Josep Bartomeu amedai si haki kumlaumu kwa kushuka kiwango chake.
Josep Bartomeu amesema: “Messi ana Mkataba hadi 2018 lakini tunataka kuuboresha na uende sawa na hali ya sasa ya Soka. Watu hawamtendei haki kumlaumu Messi. Amiongoza Barca kwenye ushindi katika Miaka mingi sasa.”
Hivi sasa kumezagaa uvumi kuwa Manchester City, na hata PSG, wanawania kumnunua Mchezaji huyo ambae anadaiwa  kutofurahishwa na Neymar kulipwa zaidi yake ingawa hili halijathibitishwa.


Lionel Messi-Msimu huu:
-Mechi: 39
-Magoli:  41

0 comments:

Post a Comment