Facebook

Monday, 21 April 2014

Moyes azidi kuwakera mashabiki,United yachapwa na Everton..................soma hapa.............

MOYES_MASIKITIKO 

Jumapili 20 Aprili 2014
Norwich 2-3 Liverpool
Hull 0-3 Arsenal
Everton 2-0 Man United

 WALIKUWA HAWAJAWAHI kuifunga Man United nje ndani kwenye Ligi tangu 1969 lakini Msimu huu Everton wamefanikiwa kuifunga Man United mara mbili na Leo ni Bao 2-0 huko Goodison Park.
Hii ni mara ya 4 tu kwa Everton kuifunga Man United katika Mechi 37 za Ligi na haya yote yanajumlisha Msimu wa aina gani David Moyes, Meneja wa zamani wa Everton aliechukua Timu ya Mabingwa Man United Msimu huu, na kuifanya ipokee kipigo cha 11 kwenye Ligi na kubakia Nafasi ya 7.
Mgoli za Everton, la kwanza  lilifungwa kwa Penati na Leighton Baines na la pili likifungwa na Mirallas, yote Kipindi cha Kwanza, na kuwaacha Washabiki wa Man United kwenye majonzi huku wakijiuliza na kuhoji upangaji wa Timu wa Moyes ambae kwenye Mechi ya 55 mfululizo hajapanga Timu ile ile na kila kukicha anabadili Kikosi

0 comments:

Post a Comment