Msanii
Maarufu nchini Tanzania Muarabu wa Dubai (a k a Mpoki) atua katika Jiji
la Frankfurt na kuelekea moja kwa moja katika Jiji la Maraha
Aschaffenburg ambapo atalala usiku mmoja na kuendelea na safari siku ya
pili kuelekea Jiji La Berlin ambapo atahudhuria mkutano mkuu wa Umoja
wa watanzania Ujerumani (U T U), kongamano la biashara pamoja
Vyanzo
vyetu vya habari vinanyetisha kwamba msanii huyo alitua katika uwanja
wa kimataifa wa Frankfurt mnamo saa 10:30 alasiri na ndege ya shirika
la ndege la Ethiopia Airlines akitokea Dar es salaam kupitia Addis
Ababa. msanii huyo alipokelewa na mwenyekiti wa watanzania nchini
ujerumani.
Tunawatakia watanzania wanaoishi ujerumani kila la heri na mafanikio katika sherehe hii kubwa na ya aina yake.
0 comments:
Post a Comment