‘VIDEO
queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’, amefunguka kuwa aliyempa
mzigo wa unga na akakamatwa nao nchini Afrika Kusini, alikuwa amevalia
kininja, hali iliyomfanya ashindwe kumtambua.
Taarifa za uhakika
kutoka vyanzo vyetu makini katika kikosi kazi cha kuzuia na kudhibiti
madawa ya kulevya nchini (Task Force), zinasema kuwa mwanadada huyo
alipofika katika nchi hiyo, alipigiwa simu na mtu ambaye hamjui
aliyemwambia kuwa atapewa mzigo, hivyo ajiandae kuupokea.“Alidai kuwa
kuna mtu aliyevalia kininja alifika eneo alilokuwepo uwanjani pale
ambaye hakumsemesha badala yake alimpatia mzigo wa unga ambao ulikuwa
kilo 150 ambao hapa kwetu ni madawa ya kulevya na kuondoka
kusikojulika,” kilisema chanzo.
Kwa upande wake, Kamanda wa
Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa
alipohojiwa na gazeti hili alithibitisha kuwa Masogange aliwaeleza
polisi wa Afrika Kusini kuwa aliyempa unga ule ni mtu aliyekuwa amevalia
kininja.“Unajua watu hawa wanaojihusisha na madawa ya kulevya wana
mbinu nyingi na wamekuwa wamejiandaa kwa lolote litakalotokea. Naamini
alisema vile ili kukwepa kushurutishwa kumtaja aliyempa. “Aliwaambia
kuwa mtu huyo alimpa mabegi yale palepale uwanjani na hawezi kumtambua
kwa sura labda kwa fulana aliyokuwa amevaa kwa sababu alikuwa amevaa
kininja,” alifafanua Kamanda Nzowa.Alisema unga huo ulifanyiwa uchunguzi
kwa mkemia mkuu wa serikali wa nchi hiyo na ikagundulika kuwa si
Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine ambayo si unga ila ni kemikali
hatari ambayo ikichanganywa na dawa nyingine hupatikana unga halisi wa
madawa ya kulevya. Aliongeza kuwa, mtu yeyote akikamatwa na malighafi
kama hizo hapa nchini adhabu yake haizidi faini ya shilingi milioni 5 au
kifungo cha miaka 30 ama zaidi. |
0 comments:
Post a Comment