Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ametishia kuwafukuza kutoka nchini humo wanadiplomasia wanaopigia debe mapenzi ya jinsia moja.
Katika hotuba yake ya sherehe za kuadhimisha
uhuru wa nchi hiyo, Mugabe alitumia fursa hiyo, kukaripia kile
alichokiita upuuzi wa nchi za ulaya zinazohubiri ushogaSio mara ya kwanza Mugabe amekemea swala la ushoga.
Aliwahi kuwataja mashoga kuwa wabaya kuliko Mbwa na Nguruwe.
Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Zimbabwe na mashoga hukamatwa mara kwa mara kwa kosa hilo.
0 comments:
Post a Comment