Facebook

Sunday, 20 April 2014

Rumminegge amtaka Ronaldo nusu fainali.......soma hapa..................

352277_heroa
MKURUGENZI Mtendaji wa Bayern Munich,  Heinz Rummenigge anahitaji kumuona mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid ambayo itatazamwa na dunia nzima.
Rummenigge amesikika akisema Ronaldo amepona majeruhi yake na anatamani kumuona katika mechi yao.
Ronaldo mwenye miaka 29 alipata majeruhi ya misuli katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund uwanja wa Santiago Bernabeu hatua ya robo fainali.
Nyota huyo hajacheza kuanzia hapo na alikosa mechi ya fainali ya kombe la Mfalme, Copa del Rey ambapo Real Madrid ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Barcelona  na kutwaa kikombe hicho.
Hata hivyo, Rummenigge ana matumaini ya kumuona nyota huyo wa zamani wa Manchester United ili kuongeza utamu wa mechi yao kama miaka ya nyuma.
“Siku zote natamani kuona wachezaji bora wakiwa uwanjani kwasababu hutua ya nusu fainali ni kubwa na inatazamwa na dunia nzima”.
“Mechi nyingine (Atletico Madrid na Chelsea) ni nzuri, lakini kama Real Madrid inacheza na Bayern Munic inakuwa mechi ya dunia nzima”.
“Napenda sana kuona wanasoka bora uwanjani, lakini kama Ronaldo atakuwepo au la, siwezi kusema sasa”. Amesema Rummenigge, mkurugenzi mtandeji wa Bayern.

0 comments:

Post a Comment