Facebook

Sunday, 20 April 2014

Mourinho ampongeza refa baada ya kichapo...........fuatilia hapa........


392947_heroa


KATIKA hali ya kuwashangaza wengi, kocha wa Chelsea Jose Mourinho baada ya kichapo cha jana cha mabao 2-1 kutoka kwa Sunderland na kuzidi kuzika matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu, amewapongeza waamuzi wa mechi hiyo.
Paka weusi walipewa penati iliyofungwa na Fabio Borini dakika za mwisho, lakini Mourinho hajalalamika juu ya maamuzi hayo badala yake amempongeza mwamuzi wa mechi.
Mourinho amewamwagia sifa mwamuzi Mike Mike Riley na msimamizi wa mechi, Mike Dean kwa kusimamia vizuri mechi hiyo.
Chelsea walianza kuandika bao la mapema kupitia kwa mkongwe, Samuel Eto`o, lakini Connor Wickham aliisawazishia Sunderland, kabla ya Fabio Borini kufunga bao lililowapatia pointi zote tatu.
Mashabiki wa Chelsea walilalamikia maamuzi ya mwamuzi.
Hata kocha msaidizi Rui Faria aligomea maamuzi hayo lakini mambo kwa bosi mkuu, Mourinho yalikuwa tofauti kabisa.
“Nina mambo manne ya kuzungumza”. Mourinho aliuambia mtandao wa michezo wa Sky Sports.
“Hongera kwa wachezaji wangu kwasababu walijitahidi wawezavyo. Hongera kwa Sunderland kwasababu wameshinda”.
“Hongera kwa Mike Dean kwasababu amefanya kazi nzuri sana. Na hongera kwa Mike Riley kwasababu amekuwa akifanya kazi nzuri katika michuano ya ligi kuu msimu huu”
“Kwahiyo hongera kwa wote na sina la kuzungumza zaidi”

0 comments:

Post a Comment