Facebook

Thursday, 24 April 2014

Shabiki wa Liverpool aliyefuga nywele miaka 11 akiapa kutokata mpaka Liverpool awe bingwa EPL.................fuatilia hapa kisa hiki.............

uka1_9644 

Shabiki wa mmoja wa klabu ya Liverpool huko nchini Kosovo ameweka kiapo kilichodumu kwa miaka 11 juu ya klabu ya Liverpool.
Shabiki huyo aliyefahamika kwa jina la Ukë Krasniqi aliweka kiapo cha kutokukata nywele zake miaka 11 –  kuanzia mwaka 2003 mpaka leo hii, akiapa kwamba hatozikata nywele hizo mpaka pale Liverpool itakapotwaa ubingwa wa Uingereza maarufu kama Barclays Premier League.
Hivi sasa story hiyo ya raia huyo wa Kosovo imetengeneza headlines na gazeti la Kosovo Republika.mk, limemfanyia mahojiano Ukë Krasniqi na haya ndio aliyosema:

“Tangu mwaka 2003 nilianza kufuga nywele zangu…Mpaka sasa Liverpool imeshinda kila kombe lakini sio Premier League. Sasa tumekaribia kushinda ubingwa huo. 
Hata kama tutangazwa mabingwa mapema, nitaendelea kufuga nywele zangu mpaka May 11. Nataka kushangilia na nywele zangu  wakati Steve Gerrard atakapobeba kombe kwa mara ya kwanza, kisha baada ya hapo nitakata.”

0 comments:

Post a Comment