Facebook

Thursday, 24 April 2014

Sitta azungumzia juu ya kauli za matusi zinazotolewa na wajumbe mbalimbali bunge la katiba..............fuatilia hapa.........................


Tumekuwa waoga sana hata tunaogopa kujadiliana ukweli, kila mtu anaogopa. Hii inaletwa na tatizo kubwa la uchumi, uhakika wa ajira, kazi na biashara za kujuana, elimu mbovu isiyoandaa watoto wetu kujitegemea.

Dodoma nyuso zote zilizobaki zinauwoga mkubwa kuliko ukweli. Haya ndio madhara makubwa uchumi kushikiliwa na serikali. Inasikitisha sana kumuona Dr mwenye PHD mwoga na muongo, sio kwamba hajui anadanganya ila ni shida ndio inamfanya muoga na mwongo. Rushwa za madaraka, ajira, biashara na tender za kujauna zinawafunga wengi jela ya uhuru, ukweli, taaluma halisi na kuwajengea watanzania na kizazi kijacho Tanzania njema.

Hatuwezi kutoka kwenye hili tope na waoga hawa tulionao. Ili tuendelee kuna kizazi lazima kipumzike. Huwezi kwenda mbele na askari anayegopa mabadiliko. Dunia inabadilika halafu sisi tunahitaji kubakia pale pale.
Ukimsikiliza kwa makini Hotuma ya Rasimu ya Jaji Warioba ilitoa mapendekezo mengi kuhusu muundo wa serikali, haikujifunga ila kila muundo unahitaji mabadiliko makubwa. Kwanini wana CCM hawataki kuujadili muundo wanaoupenda kwa kuzingatia maoni na uwasilishaji wa Rasimu?

Kama kweli nia ni serikali mbili kwanini wasiseme wazi, katiba ya sasa ya zanzibar is invalid, haipo haitambuliki, wasiseme turudi kwenye seikali moja yenye nchi mbili? Kwanini wasiseme mabadiliko yote yaliyofanywa kinyemela yamekiuka katiba na hayatambuliki pande zote bara na visiwani?
Kwa nini wasikubali kujadili kwa kina mambo yote yaliyouwa muungano wa serikali moja? Kwa nini wasijadili ilikuwaje zanzibar ikawa nchi na katiba yake kinyume cha makubaliano ya Muungano? Kwanini wasijadili kwanini Raisi wa Muungano sio raisi wa Zanzibar tena? 

Nataka Dr Mwakyembe mwanasheria, Andrew Chenge, Nimrod Mkono, Werema, Sita, na wanasheria wote nguli wa CCM waache mipasho warudie taaluma zao wapambane hoja kwa hoja. Yuko wapi Asha Rose wa Migiro, Vijana wasomi kama Januari makamba, Mo, mko wapi mnaogopa kuitetea serikali yenu kwa ukweli na uwazi?
Samweli Sita azuie mipasho , taarabu, matusi, lugha za kebehi watu wajenge hoja na kushindana kwa facts. Wananchi tusikilize wachambue ukweli, then tuambiwe tupige kura kutokana na debate chanya. 

Hata kama wafuasi na wajumbe wa chama tawala hawataki, wajumbe wa Ukawa wamejipanga kwa data, facts, na jinsi wanavyojenga hoja, Pamoja na kwamba wajumbe wa CCM wamebaki wenyewe wameshindwa kushawishi umma kwa nini wanataka serikali mbili. Kama kweli kina Mwakyembe wangekuwa na hoja za ushindi huu ndio ungekuwa muda wa kushinda kwa hoja kwani wote wanatetea serikali mbili ndani ya mjengo. Wananchi ni mashahidi wameshindwa wameishia kutukana hewa. Ukawa hawapo ndani kila mchangiaji anatukana member ambao hawapo.

Leo hii kila anayesimama anatukana mtu.

Kama wanaCCM na wajumbe wao wangejua hakuna katiba ya Ukawa wala ya CCM bali ya Tanzania, wasingeleta fujo na kulazimisha kujadili rasimu ya CCM. Lazima tuijadili rasimu ya warioba ama tuikubali kwa hoja ama tuikatae kwa hoja then tuipigie kura.

CCM wajipange wawape mijadala hii wanaCCM wenye akili timamu na ufahamu ili wapambane na akina Lissu, Zito, Kafulila, Lipumba, Mbatia, Jusa, nk. Team ya ukawa imejipanga kiuchumi, kisheria, kijamii, kisayansi, kisiasa, diplomasia, nk nk. CCM inabidi wa-copy jinsi ya kufanya kazi. Kusimamisha vidosho kuchangia matusi na lugha za kubagua watanzania na uchochezi wa kijeshi haziwezi kusaidia.

0 comments:

Post a Comment