KOCHA
wa Atletico Madrid, Diego Simeone ameieleza suluhu ya leo dhidi ya
Chelsea kuwa imewapa unafuu mkubwa wapinzani wake kuelekea katika mchezo
wa marudiano nchini England.
Vinara
hao wa La Liga walicheza mpira mzuri, lakini walishindwa kupenya ngoma
ya ulinzi ya Chelsea licha ya krosi nyingi kupigwa katika eneo la hatari
la the Blues.
Diego
Costa alishindwa kufanya maarifa ya kufunga kipindi cha kwanza, wakati
mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha Gabi uliokolewa vizuri na kipa
aliyeingia kuchukua nafasi ya Cech, Mark Schwarzer.
Beki
na nahodha wa Chelsea, John Terry alitoka kipindi cha pili baada ya
kupata majeruhi ya enka, lakini Simeone anaamini wapinzani wake watakuwa
na furaha zaidi kwao Stamford Bridge wiki ijayo.
“Ulikuwa mchezo mgumu na kila mtu alishindwa kupata matokeo” Alisema Margenina huyo.
“Tulishindwa kupata bao la ushindi. Ilikuwa mechi ngumu kwa timu zote kwasababu zinapambana kufika fainali”.
“Wana faida na suluhu hii, lakini yeyote atakayeshinda mechi ijayo ataenda fainali”.
0 comments:
Post a Comment