JOSE
Mourinho amethibitisha kuwa Peter Cech atakosa mechi zote zilizosalia
msimu huu baada ya kuteguka bega, lakini amesisitiza kuwa Chelsea
inahitaji kufika fainali ili John Terry apate nafasi ya kucheza tena.
Cech
aligongana na Raul Garcia kipindi cha kwanza katika suluhu ya bila
kufungana na Atletico Madrid na alipelekwa moja kwa moja hospitali
kupimwa.
Wakati huo huo, Terry aliumia kifundo cha mguu baada ya kukanyagwa na Diego Costa katika dakika ya 71.
Nahodha huyo wa Chelsea alijitahidi kuendelea kucheza lakini alishindwa na kutoka.
“Peter Cech msimu kwake umekwisha” Mourinho amewaambia waandishi wa habari baada ya mechi.
“Kwa John (Terry), tunatakiwa kucheza fainali ili acheze tena”.
Terry
na Cech watakosa mechi ngumu ya ligi kuu England dhidi ya Liverpool
katika uwanja wa Anfield jumapili ya wiki hii na mechi ya marudiano na
Atletico aprili 30 mwaka huu darajani.
John Obi Mikel na Frank Lampard watakosa mechi ya marudiano kufuatia kupata kadi mbili za njano, lakini Branislav Ivanovic atakuwepo baada ya kumaliza adhabu yake ya kusimamishwa.
0 comments:
Post a Comment