Viongozi wa mashitaka nchini
Korea Kusini wameiomba mahakama kutoa kibali cha kukamatwa kwa nahodha
wa feri ya abiria iliyozama siku ya Jumatano ikiwa imewabeba zaidi ya
watu 400.
Hadi kufikia sasa watu mia mbili na sabini hawajulikani waliko.Mmoja wa wapiga mbizi hao alisema kuwa hawakufanikiwa kuiona vizuri feri hiyo hali iliyowalazimu kuiguza kwa mikono yao.
Afisa wa ulinzi wa Pwani,Ko Myung Suk amesema kuwa hawakupata manusura yeyote eneo walilofanikiwa kufika.
Naibu mwalimu mkuu kwenye shule ambapo wengi wa wanafunzi walikuwa wakisomea amepatikana akiwa ameaga dunia.
Vyombo vya habari vinasema kuwa huenda mwalimu huyo amejitoa uhai.
0 comments:
Post a Comment